Baadhi ya vyumba vya madarasa kikiwemo chumba cha
kuhifadhia vitabu katika shule ya msingi Daraja mbili iliyoko jijini
Arusha vimeteketea kwa moto ambao bado chanzo chake hakijajulikana.
Baadhi ya Majengo ya Shule ya Msingi Daraja mbili yaliyotketea kwa moto
Pia
moto huo umeteketeza kadi za taarifa za maendeleo ya wanafunzi, ikiwa
ni masaa machache kwa moto huo kutokea mara baada ya kufungwa kwa shule
hiyo kwa likizo ya mwisho wa mwaka.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Steven Kweka amesema kwa sasa bado
hawajafanya tathmini kujua thamani ya vitu vilivyoteketea ila anaomba
jitihada za haraka zifanyike kuzuia athari zinazoweza kutokea kutokana
na tukio hilo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkurlu ametembelea etembelea shuleni
hapo amesema tayari amewaagiza waandisi kufanya tathmini ya vyumba
vilivyoungua kwa lengo la kuanza ukarabati, pia ametoa wito kwa
wananchi na taasisi kujitokeza kuchangia shule hiyo
No comments:
Post a Comment