Muigizaji anayezidi kujitengenezea jina kupitia
fani ya uigizaji filamu nchini mwanadada Rachel Bithulo, yupo katika
mchakato wa kumalizia kuigiza katika filamu mpya iliyobatizwa jina 'Dead
Samson'.

Muigizaji wa filamu nchini mwanadada Rachel Bithulo
Rachel
ameongea na enewz kuwa hii ni moja kati ya filamu ambayo ameonesha
uwezo wake mahiri akikiri kuwa ameweza kuimarika na kuungana na
waigizaji nyota nchini wakiwemo Ahmed Makambaza, Albert Thadei na wakali
wengine kama Awadhi na Sogadi.
Rachel aongea na enewz kuhusiana na filamu hiyo mpya ya 'Dead Samson'
inayotarajiwa kuwafikia mashabiki na wadau wa filamu kuanzia mwanzoni
mwa mwaka 2016, huku akiwa tayari ameigiza filamu maarufu kama 'Kidudu
Mtu', 'Claritha', 'Why Me', na nyinginezo nyingi.
No comments:
Post a Comment