Aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, Lazaro
Nyalandu, amepongeza uteuzi wa Prof. Jumanne Maghembe, kuwa Waziri wa
wizara hiyo, akisema ni kiongozi makini na mchapakazi.
Amesema ana imani kubwa Prof. Maghembe ataendeleza mapambano dhidi ya
majangili wanaoua wanyamapori katika hifadhi za taifa na mapori ya akiba
nchini.
Pia, amepongeza kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli, kuwa imeamsha matumaini ya Watanzania na kwamba kama Ilani ya Uchaguzi ya CCM inavyoeleza, atashirikiano nayo bega kwa bega ili kuijenga Tanzania mpya.
Nyalandu alisema hayo jana wakati akizungumzia uteuzi wa Prof. Maghembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

“Prof. Maghembe ni msomi, mtu makini na mwenye kuifahamu vyema wizara ile (Maliasili na Utalii) kwa sababu aliwahi kuongoza kabla yangu. Nimefanya kazi zangu vizuri nikiwa pale kwa sababu kuna misingi imara aliiweka wakati wa uongozi wake.
Dk. Magufuli amefanya uteuzi makini,” alisema Nyalandu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Kaskazini.
Alisema hana shaka Prof. Maghembe ataendelea kukuza uhifadhi endelevu na kuvutia watalii nchini.
Kuhusu utendaji wa serikali ya Dk. Magufuli, Nyalandu alisema imeanza na kasi nzuri na kurejesha imani na matumaini ya Watanzania kuwa CCM imeendelea kutoa hazina ya viongozi wa kuliongoza taifa.
Alisema Dk. Magufuli alieleza dhamira yake ya kuijenga Tanzania mpya tangu wakati wa kampeni, kinachoendelea kwa sasa ni utekelezaji wake.
“Wazembe walioanza kuwajibishwa watafikisha salamu kwa wenzao na lengo ni kuhakikisha kunakuwa na nidhamu katika utumishi wa umma.
Kila mtumishi yuko kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania, hivyo suala la msingi ni kumuunga mkono Dk. Magufuli na kumuombea,” alisema Nyalandu.

No comments:
Post a Comment