TTCL

EQUITY

Friday, December 25, 2015

Kasi ya Magufuli, Majaliwa yastua CCM, upinzani

Kasi waliyoanza nayo Kasi waliyoanza nayo Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambao wanaweza kupewa jina la ‘M kipeo cha pili’ (M2) ya kutumbua majipu ya mafisadi na wakwepa kodi, huenda ikaibua upinzani ndani ya CCM. 
 
Hofu imetanda miongoni mwa baadhi ya wana CCM na wale wa kambi ya upinzani wasiopenda mabadiliko na ambao kwa namna moja au nyingine huenda maslahi yao binafsi yataguswa na kasi hiyo. Katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida wanachama hao wanaangalia namna ya kudhoofisha juhudi hizo zilizoanzishwa na Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Adui wa kwanza anatoka ndani ya chama chake (CCM) na wa pili anaibuka kutoka kambi ya upinzani. Shabaha ya vita hivi huenda ni kutaka kuhujumu nguvu za Rais Magufuli na ili operasheni hii isije kuwagusa na kuwaumiza  vigogo wa  pande zote mbili. 
 
Nikianza na adui wa ndani, itakumbukwa kwamba katika kipindi cha kampeni, kambi zote mbili zilikuwa na ajenda kuu ya “mabadiliko” hata hivyo dhima ya kupinga ufisadi na rushwa ilikuwa ni shabaha kubwa ya wapinzani.
 
Tangu Rais Mafuguli achukue uongozi, mara moja alianza kuonyesha dhamira yake kwa vitendo pale alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na Wizara ya Fedha. Kwenye ziara hizo alimuondoa Kaimu Mkurugenzi wa Muhimbili, Dk. Hussein Kidanto na kusitisha bodi nzima ya wakurugenzi. 
 
Siku chache baada ya Rais Magufuli kuacha kilio kwenye ziara yake, Waziri Mkuu alifuata nyayo na kuzitembelea ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA), ambapo matokeo yake yalikuwa ni kusimamishwa kazi kwa makamishna watano akiwamo Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade, baada ya kugundulika ufisadi mkubwa wa kukwepa kodi kwenye makotena yanayopita bandarini.
 
Kutokana na hatua hizo za Rais Magufuli za kuanza kutumbua majipu, kunahofu huenda atawagusa baadhi ya wana CCM. Kuna hofu kuwa ndani wapo baadhi ya wananchama wasiokuwa waaminifu ambao wameanza kujenga hoja kuwa endapo hatadhibitiwa mapema, basi mambo yatakwenda mrama kwani chama hicho kimekuwa kikinufaika na misaada kutoka kwa wafadhili wanaokabiliwa na tuhuma za ukwepaji wa kodi. 
 
Inahofiwa Rais Magufuli asipodhitibiwa mapema na chama, ipo siku ataingilia makampuni yaliyoanzishwa na chama siku za nyuma na kuhusishwa na ufisadi, kwa mfano Meremeta.
 
Inahofiwa kuwa rungu lake likifikia maeneo hayo, CCM itakuwa imevuliwa nguo na kwamba hakuna kiongozi wa CCM atakayesalimika pale atakapoanza kutumbua jipu la makampuni hayo na yale yaliyoanza kusaulika mfano kashifa ya akaunti ya madeni ya nje (EPA).
 
Kwa msingi huo, vita vilivyoanza ndani ya chama hicho ni kutaka kumfunda Rais Magufuli ili asichokonoe yaliyopita. Kwanza aanzie hapa alikoishia mtangulizi wake. Asahau yaliyopita vinginevyo atatumbua makovu ya majipu ambayo huenda hata yeye akashindwa kumpata daktari wa kuyatibu.
 
Ninachotaka kusema ni kwamba kuna baadhi ya viongozi ndani ya CCM ambao walihusika kwa njia moja au nyingine kutoa vibali na ‘vimemo’ kwa wafanyabiashara wakubwa ambao wamekuwa wakivitumia kukwepa kulipa kodi za serikali kwa maslahi binafsi. Hivyo kasi hii ya Rais itawaumbua hadharani. 
 
Kwa kutambua hali hiyo, vigogo hao wameanzisha ushirika bubu na kambi ya upinzani ili kwa pamoja watafute mbinu za kuhujumu nguvu hizo za Rais Magufuli. Wanadai eti hatafanikiwa bila ya kuungwa mkono na wana CCM wenzake. 
 
Vita vya pili vinahusu kambi ya upinzani. Mtoa taarifa alisema kwamba, kambi ya upinzani nako hakuna usalama. Inaelezwa kuwa wapo baadhi ya vigogo waliopo kambi hiyo ya upinzani ambao pia wana mahusiano na wakwepa kodi. 
 
Inasemekana baadhi ya viongozi kutoka kambi ya chama tawala wanawapa nguvu wapinzani ili wamchefue Rais Magufuli kwa madai kwamba anafanya kazi ya “One man show” yaani kazi bila ushirikiano na wenzake. 
 
Kuna madai kuwa Rais Magufuli haambiliki, hashauriki, hasikii ya mtu, hivyo anaweza kuleta madhara kwa taifa. Kauli mbiu yao ni kufuta agenda ya mabadiliko na mbadala wake kuingiza agenda ya “katiba mpya” na kutangazwa kwa matokeo ya Zanzibar. 
 
"Jamaa atalazimika kujieleza kwenye kelele za wapinzani hivyo agenda yake ya mabadiliko itakufa tu” alisema mtoa taarifa. Kimsingi vita hivi vinataka kumtoa Rais Magufuli nje ya reli ili aachane na hoja ya kutumbua majipu. Hata hivyo, wapiganaji wa vita hivyo wanaogopa nguvu za Umma iliyopo nyuma. Tusubiri.
 
Mawasiliano:0713 399004/0767 399004,"mailto:jmkibasso@gmail.com" jmkibasso@gmail.com , ambao wanaweza kupewa jina la ‘M kipeo cha pili’ (M2) ya kutumbua majipu ya mafisadi na wakwepa kodi, huenda ikaibua upinzani ndani ya CCM. 
 
No comments:

Post a Comment