
Mtu
mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja aliejifanya Afisawa
mamlaka ya mapato - TRA aliyekuwa na gari lenye namba za usajili T945
BYG amenusurika kifo mara baada ya kula kichapo kutoka kwa wananchi
wakati akiwa kwenye harakati za kufanya utapeli kwenye duka kubwa la VEW
POINT lililopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa duka hilo mtu huyo aliejifanya afisa
kutoka mamlaka ya mapato TRA sio mara ya kwanza kufika eneo hilo kwani
siku moja kabla alifika akiwa na wenzake wawili na mmoja
waliyemtambulisha kuwa ni mwandishi wa habari na kufanikiwa kutapeli
kiasi cha shilingi milioni tano.
Mtuhumiwa huyo sasa amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi Tabata Segerea kwa hatua zaidi za Kisheria.
No comments:
Post a Comment