TTCL

EQUITY

Sunday, November 30, 2014

HOJA YA MASOUD KIPANYA KUHUSU SAKATA LA IPTL & ESCROW

Masoud Kipanya Anasema:- asante wabunge (hasa) wa upinzani kwa jana kutulindia heshima yetu kama nchi, asante watanzania mliolishupalia japo kwa kulifuatilia sakata la ESKELEWU, najisikia fahari kuirudia hapa chini post hii ya 26/10/2014, samaki wengi wamelia kwa pamoja, machozi yamefurikisha maji. Tusiache kulia zaidi, Halmashauri zetu ZINANUKA! 
"Samaki mmoja akilia machozi hupotea.
Samaki wote, wa bahari zote, mito na vijito vyote, maziwa yote na madimbwi yote duniani, wakikubaliana kulia kwa pa...moja kwa wakati mmoja, (Hypothetically) wanaweza kusababisha Dunia ikafurika kutokana na kuongeza kina cha maji yatakayokutana kutokea baharini, maziwani, mitoni, na kote kuliko na samaki. 
Sakata la IPTL na ESCROW kwa watanzania walio wengi ni sawa na Mwanafunzi wa darasa la pili anayesikia hesabu za 'Pai mara Kipenyo zidisha na Y kupata thamani ya X' kwa kifupi watanzania WENGI hawaelewi.
Nakuomba mheshimiwa Zitto Kabwe na wengineo wenye ufahamu wa jambo Hili, watumie lugha rahisi na fupi na ikibidi na mifano ili kuwafafanulia watanzania ili badala ya kuwaacha samaki wachache walie huku machozi yakipotea, TULIE WOTE KWA PAMOJA TUWEZE KULETA MAFURIKO (IMPACT)".


 

No comments:

Post a Comment