Mke wa aliyekuwa
mgombea wa urais kupitia chama cha CHADEMA nchini Tanzania Edward
Lowassa amekataa ombi la kamati ya chama hicho kumpatia ubunge wa viti
maalum.
Taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na msemaji wa
Lowassa Abubakar Liongo imesema kuwa bi. Regina Lowassa aliikataa nafasi
hiyo kwa nia njema.
Bwana Liongo amesisitiza kuwa bi. Regina
ataendelea kuwahudumia raia hususan wanawake hata ijapokuwa ameikataa
fursa hiyo ya kuwa mbunge.
''Naishukuru kamati ya chama changu kwa
kunipatia heshima hiyo lakini sijaikubali.Nadhani itakuwa nyema kwangu
mimi kuendelea na harakati zangu kuwapigania raia hususan wanawake
nikiwa nje ya bunge''alisema.
Kamati kuu ya CHADEMA ilimpatia nafasi hiyo kutokana na mchango wake katika kampeni ambao ulisaidia kupatikana kwa majimbo.
No comments:
Post a Comment