TTCL

EQUITY

Sunday, October 4, 2015

MELANCE KINABO NI MFANISI NA MAKINI


 

Akiwa Diwani mteule wa kata ya Themi Jimbo la Arusha Mjini 2013 Ndugu Melance Kinabo (KABURU) kupitia CHADEMA, Kwa uchungu mkubwa alianza kazi zake rasmi kama diwani hili hali bado hakuwa ameapishwa.Leo tarehe 29 - June 2013 mishale ya saa tisa alasiri na kuwasili mtaa wa Fire maeneo ya magorofa ya polisi kusikiliza kilio cha akina mama ambao ni wakulima wa mbogamboga waliomuita kwa simu kumuomba msaada baada ya mwenyekiti wa Mtaa wa Themi Magharibi Mzee Dions Msele - CCM kukataza matumizi ya mfereji wa kumwagia maji ktk mashamba ya kina mama wa mtaa husika bila sababu za msingi.

 

Diwani huyu wa Themi kupitia Chadema  aliwahoji akina mama husika na kugundua kuwa Mwenyikiti wa mtaa hakuwa na sababu za msingi za kuwazuiya kina mama hao kuendelea na kilimo cha umwagiliaji kupitia mfereji husika.


Diwani huyu mteulealipofika kwa mtendaji wa kata ya Themi aligundua kuwa kina mama hawa wa Themi Magharibi wananyanyaswa na mwenyekiti wa mtaa Dions Msele - CCM na ndipo akatoa amri kuwa mfereji huo ufunguliwe na kina mama waendelee na kilimo cha mboga bila kusumbuliwa na kutoa ahadi ya kusimamia utengenezaji wa kalavat kwenye mfereji husika kuepusha ajali kwa watoto wa polisi wanaoishi maeneo ya Themi Magharibi karibu na chanzo cha mfereji huo ulioleta utata jambo ambalo limekwisha shughulikiwa.

Aidha mwanachi mmoja amabaye hakutaka jina lake litajwe wakati akihojiana na mwandishi wetu alisema kuwa wananchi wa Arusha wanajua Rais ni Lowassa, Mbunge ni Lema na Diwani wa Themi ni Melance Kinabo, hakuna asiyejua ufanisi na umakini wake wa utendaji, niseme tu viongozi hawa ni wawajibikaji, wazalendo na watu makini.
  
 
Hivi ni moja ya vipaumbele vya Mh. Kinabo katika ahadi zake iwapo wananchi watampa ridhaa tena ya kuwaongoza na kuwa Diwani wa kata ya Themi mwaka 2015-2020.
  • AFYA
Kujenga uzio na kukamilisha maboresho yote ya kituo cha Afya Themi, ikiwemo ujenzi na ufungaji mashine ya kuchoma taka za Hospitali, ujenzi wa chumba cha upasuaji kina mama wajawazito, na ununuzi wa Gari la wagonjwa (Ambulance).
  • MIUNDOMBINU NA MIPANGO MIJI
 Upatikanaji wa maeneo ya wazi kwajili ya biashara za vijana na akinamama. Kupata upimaji wa maeneo mbalimbali ndani ya kata ( Mtaa wa Kambarage), ukarabati na ujenzi wa barabara zote za kata, ikiwemo Serengeti (mtaa Corridor area, pamojana Engira road, na Barabara za AICC Flats), kufungua barabara zinazounganisha kati ya mtaa kwa mtaa na kata kwa kata. kuongeza nguvu za kisheria katika kuimarisha na kuboresha miundombinu ya AICC barabara na nyumba, pia upatikanaji wa maji safi  na salama kwa uhakika, mfano mtaa wa AICC, Themi mashariki na Kambarage. Aidha kujenga, na kutetea kwa nguvu zote hoja  ya ukarabati wa nyumba za polisi (Old polisi fire) chombo ambacho ni muhimu sana kwa raia na mali zao. 
  • ELIMU
Jinsi ya kumsaidia Mtanzania ni kumpa Elimu.  Alisema Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh. Cristopher Kongoye alipokuwa akimshukuru Mh. Diwani wa Themi Melance Edmund Kinabo na kuungana nae kwa kusema, tunawaitaji watu wanaoleta maendelea kama wewe na kumwaidi kumpa ushirikiano wa kutosha na kusema hataitaji watu mizigo kwenye maendeleo.
Kwakutambua hilo, Mh. Kinabo ameongeza msimamo wake na kuahidi kusimamia upatikanajii wa shule ya ufundi kwaajili ya vijana katika shule ya msingi Engira.
Ufuatiliaji na usimamizi thabiti ili kupatikana kwa eneo la ujenzi wa shule ya msingi kati ya kata ya Engutoto na Mtaa wa kambarage.
Ujenzi wa ukuta wa shule ya msingi Engira pamoja na kukamilisha ujenzi na ukarabati wa Shule ya sekondari Themi na shule ya msingi Themi.
Kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda shule.

 
  • UCHUMI
Kuwezesha vikundi vya  VICOBA kuwa SACCOSS
Kuanzisha/ kuunda kongamano la mafunzo kwaajili ya vijana (Ujasiriamali)
Kutambua makundi maalum na kuweza kuwasaidia
Kuunda timu ya soka kata ya Themi.
  • ULINZI NA USALAMA
 Kuhakikisha kuwa vinaundwa vikundi vya vijana kwaajili ya ulinzi shirikishi, ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ndani ya kata ya Themi.

No comments:

Post a Comment