TTCL

EQUITY

Saturday, October 3, 2015

BREAKING: Mchungaji Christopher Mtikila wa DP amefariki.

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha  DP Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.

IMG-20151004-WA0009
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12 kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.

IMG-20151004-WA0006
Gari aliyopata nayo ajali Mch.Christopher Mtikila

Mtikila alitangaza kugombea Urais kupitia chama chake cha DP lakini chama chake ni moja ya vyama ambavyo vilikatwa kutokana na kutotimiza masharti ya uchaguzi.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment