TTCL

EQUITY

Thursday, April 2, 2015

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWA ARUSHA CHAVUNJIKA

kikao cha baraza la madiwani kimevunjika leo na kuahirishwa hadi week 
ijayo. Sababu iliyopelekea hali hiyo ni hatua ya 
madiwani chadema kutoa hoja ya kutojadiliwa 
kabrasha hadi hapo hoja zake mbili 
zitakapojadiliwa. Hoja za Nanyaro ambazo 
ziliungwa mkono na madiwani wenzake wa 
CHADEMA ni:


1:Vifaa vya zaidi ya 500mil vilivyoibwa na 
aliyekuwa daktari wa jiji virejeshwe na mwizi 
akamatwe.
2:database ya mapato 
Alisema swala la vifaa vya Levolosi na Data 
base ya zaidi ya miaka miitatu amekuwa 
akitaka hatua zichukuliwe ila hadi sasa hakuna 
chochote badala yake mkurugenzi wa jiji 
amekuwa sehemu ya tatizo. Kwa msisitizo 
akasema, taarifa za baraza yaani kabrasha limejaa 
uongo na halifai kujadiliwa.

Baada ya hoja hiyo 
diwani Doita aliunga mkono kisha kufuatiwa na 
madiwani wote wa CHADEMA hali ambayo ilimlazimu
mwenyekiti wa kikao kuahirisha kikao kwa 
muda.

Baada ya muda madiwani wote wa CHADEMA wakipaza sauti zao kwa umoja wao 
walisisitiza kutokuendelea na kikao hadi hapo 
nidhamu na uwajibikaji wa mkurugenzi na 
watu wake kwa manufaa ya wananchi wa 
Arusha Msimamo wa CHADEMA hasa kwenye swala la 
mapato ya jiji ni kuwa Jiji lina uwezo wa 
kukusanya zaidi ya mapato ya sasa licha ya 
mafanikio makubwa ya makusanyo ya 1.2 Bil 
kwa mwezi kutoka 400 mil awali. Pia makusanyo 
haya yawe kwa njia ya electronic.

No comments:

Post a Comment