TTCL

EQUITY

Thursday, April 2, 2015

KURA YA MAONI YA KATIBA MPYA...

1. Kama BVR moja (1) inaandikisha watu 80 kwa siku moja, BVR 138 (zinazofanya kazi field) zitaandikisha watu 11,040 kwa siku 1 na hiyo ina maana kuwa BVR hizo zitaandikisha watu milioni 25 (wanaopaswa kuandikishwa) kwa kutumia siku 2264 (zaidi ya miaka 6),
2. Kama BVR zote 250 zilizopo zitatumika kuandikisha, tutatumia siku 1250 (zaidi ya miaka 4),
3. Kama tutajikongoja tukaingiza walau BVR 1000 kati ya 8000 zinazohitajika ina maana tutatumia siku 312 (Takribani mwaka 1),
4. Kama tutajitahidi tukaingiza walau BVR 3000 kati ya 8000 zinazohitajika ina maana tutakamilisha uandikishaji kwa siku 104 (Takribani robo mwaka),
5. Kama tutaweza kuingiza walau BVR 5000 kati ya 8000 zinazohitajika ina maana tutakamilisha uandikishaji kwa siku 62 (Walau miezi miwili),
Aidha tuombe MUNGU...!!
Tuombe mungu kwamba bahati namba 5 imetuangukia (kwamba Mungu ametushushia BVR 5000 leo),
(a) Tukizitumia tutamaliza uandikishaji tarehe 30 Mei
(b) Kisha tutahitaji walau siku 30 za kurekebisha daftari na malalamiko ya walioandikishwa kimakosa, wasioandikishwa n.k (Itatupeleka tarehe 30 Juni).
(c) Pia tutahitaji siku zingine 60 za elimu na kampeni (zitatupeleka tarehe 30 Agosti).
(d) Hii ina maana kuwa kama tunahitaji kupiga kura ya maoni itafanyika tarehe za mwanzo za mwezi Septemba.
JE TUMECHANGANYIKIWA NA HATULIONI HILI??
Je, Tume ya Taifa ya Uchaguzi itafanya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu lini? Au tumeamua kuahirisha Uchaguzi Mkuu ili kutengeneza LEGACY ya Bwana Mkubwa kwenye katiba mpya?
Au tunataka kuunda serikali ya mseto mwezi Oktoba maana hakuna atakayekubali JK aendelee kukaa madarakani kwa sababu uchaguzi umeahirishwa? Au ndiyo ule msemo wa kuikabidhi nchi kwa Jeshi?
Mihimili hii mitatu Serikali, Bunge, na Mahakama ilikuwa wapi.!? viongozi, taasisi na watu mbalimbali waliliona hili, kwanini serikali haikuliona hili mapema, na hata hivyo kwanini ushauri wao mliuupuza..!?
Lakini leo naipongeza tume kwa maamuzi yake makini, lakini pia naamini sio maamuzi bayana, bali kutokana na kukwepa fedhea imelazimu kutekekeleza lile lililo onwa mapema na watu makini. napendekeza nivyema kupokea shauri, japo inasemwa kuwa "akili ya kuambiwa + na yakwako utapata jawabu sahihi" ushauri huu ulifaa mapema na ni sahihi, kwakua utapisha uchaguzi mkuu na shughuli nyingine kendelea.

No comments:

Post a Comment