TTCL

EQUITY

Wednesday, October 29, 2014

IYF TUMAINI JIPYA LA VIJANA



Hawa ni moja kati aya vijana walio onesha umahiri wa kujieleza na kuelezea mada zilizo kuwa na tija kwa jamii, katika shindano la IYF English Speech, na kuweza kuwa washindi ambapo walijinyakulia simu na kamera za kisasa.

Vijana ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu, na ni muhimu vijana wakatambua hilo kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii inayowazunguka. maneno hayo yaliwahi kusemwa na Dkt. Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa mara ya kwanza alipo alikwa katika ufunguzi wa kambi ya mafunzo ya vijana IYF yaliyo fanyika  August 9 2012 Jijini Dr es salaam. Tanzania ni nchi yenye vijana wengi wasio na ajira lakini wenye vipaji, huku baadhi yao wakiwa hawana ujuzi na kutojua lugha za kimataifa.

IYF (International Youth Fellowship) ni shirika la vijana linalofanya kazi kwakushirikiana na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, na yenye makao makuu yake nchini korea ya kusini, lakini ikiwa zaidi ya nchi 80 duniani.


Taasisi hii imekuwa ikiwaweka vijana pamoja kwa kuandaa kambi ikiwa lengo ni kutoa mafunzo mbalimbali kwa hususa ni Lugha (kichina, kikorea, kiingereza, kitailand), burudani na michezo (kuimba, kucheza, kutumia vifaa vya muziki), saana ya ngumi (Taekwo ndo), elimu ya dini,  michezo na elimu ya ufahamu, mashindano ya uwasilishi wa mada mbalimbali kwa lugha ya kiingereza (public speaking).



IYF ambayo imezoeleka kuitwa English Camp Msimu huu 2014 iliandaa, Elimu na michezo ya Ufahamu, lugha, elimu kuhusu dini, na uwasilishaji wa mada kwa kingereza, ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza aliibuka msichana, kwakutoa mada nzito iliyohusisha siasa na maendeleo ya vijana na mshindi wa pili alikuwa Bwa. Elvis Eliphaz aliyewatoa wanaume kimasomaso.Bi. Rogathe Manasseh Loakaki anayesoma kidato cha Tano shule ya Cornestone High School akitokea Sanawari ni binti pekee aliyeonesha kujiamini, akizungumza kwa vitendo huku akitumia mifano mbalimbali na kufanya umati wa watu kuwa makini mkusikiliza, zaidi aliibua hisia za watu pale alipotajwa kuwa mshindi wa kwanza na kuwafanya wasichana kuona kuwa wanaweza, kilichonipa ushindi ni Mungu, wala sio kwa akili zangu pekee, kujiamini na kushirikisha wengine kulinipa uwezo zaidi.




Aidha malengo ya IYF ni kuwaweka vija wa kitaifa na kimataifa pamoja na kuleta ushirikiano kati yao, ili kuleta nguvu ya ufikiri pamoja kama leo hapa tumekuwa na vijana wa Arusha, wengine wanatoka nje ya Arusha na wengine kutoka nje ya nchi, kwa kusanyiko letu tunapata ufahamu tofauti, pamoja na kumjua Mungu. Ni Oresto Adam Mwanachama na kiongozi wa IYF Ambapo alikuwa akizungumza nami.



Program hii hufanyika mara moja kwa mwaka kwa kila mkoa, na hadi sasa imefanyika Mbeya, Arusha na Dar es salaam, ambapo lengo ni kuweza kuifikia Tanzania nzima na dunia kwa ujumla. Vilevile kuna program hii ya World Camp ambapo hufanyika Dar es salaam na kukusanya vijana kutoka wilaya, na mikoa tofauti , pamoja na wengine kutoka nje ya nchi.

Pia kutoka na kuwepo kwa program nyingi pia tunayo ingine ya kimataifa hii inatwa Good News Cops (GNC) hii inatoa fursa kwa vijana kwenda kujifunza na kufundisha mataifa mengine, na kushiriki katika kujifunza namna wengine walivyo piga hatua, na msimu wapili wa GNC utafanyika wiki ijayo katika viwanja vya Mbezi Beach Jijini Dar es salaam 27 Oct. 2014

No comments:

Post a Comment