TTCL

EQUITY

Monday, December 2, 2013

Vituko vya kufunga mwaka Jamaa Mmoja na Kisa Cha Nyumba Ndogo..

Kichekesho cha Jamaa Mmoja na Nyumba Ndogo

Kuna jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa na mke mdogo kwa siri katika jiji la ...... Siku moja katika kutenga muda wa kutosha wa kujirusha na bi mdogo jamaa kapanga safari ya kikazi na kumuaga mke wake kuwa anakwenda Arusha kikazi wiki nzima. Kumbe huku nyuma alipanga kutanua na bi mdogo.
Baada ya starehe za usiku wa jana yake na bi mdogo huyo, jamaa akiwa ofisini aliamua kumtumia ujumbe wa simu nakushukuru bi mdogo
Jamaa katuma ujumbe huu;
“Asante baby kwa staili ya jana, ilikuwa kali sana na nimeipenda. Ndio maana nakupenda wewe kuliko wanawake wote duniani” >>>> na kuituma.
Baada ya kutuma jamaa kagundua kakosea namba na ilienda kwa waifu, yaani kwa mke wa ndoa
Jamaa katika kuhaha kuzuia ujumbe usimfikie mke wake alikwenda kwa wahudumu wa mtandao wa simu ili kuomba msaada wa kuzuia meseji na mazungumzo yakawa hivi:
Jamaa: Kuna meseji nilikuwa niitume kwa bi mdogo kwa bahati mbaya imekwenda kwa waifu wangu, je mnaweza kuizuia?
Mhudumu: Wahi fasta kwenye mnara ukaizuie....

No comments:

Post a Comment