TTCL

EQUITY

Tuesday, January 12, 2016

Chadema watuma salamu za rambirambi kifo cha Leticia Nyerere

8-chadema 

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA LETICIA NYERERE
Tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Mhe. Leticia Nyerere uliotokea nchini Marekani.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na mpendwa wao.
Mwenyezi Mungu awatie moyo wa ujasiri na subra katika wakati huu mgumu wa majonzi ya msiba huo.
Kama chama tutamkumbuka Marehemu Leticia kwa mchango wake na ushiriki wake wakati wote alipokuwa mwanachama wetu na akiwa miongoni mwa watu waliopata fursa za kuwa wabunge kupitia CHADEMA.
Bwana alitoa, bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.
Imetolewa leo, Jumanne Januari 12, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kisha kurejea CCM ,Leticia Nyerere aliyefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani unatariwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza leo nyumbani kwa Mama Maria Nyerere jijini Dar es salaam, msemaji wa familia Joseph Butiku amesema taratibu za kuanza kuusafirisha mwili wa marehemu zinaendelea huko nchini Marekani.
Butiku ameongeza kusema kuwa mara mwili huo utakapowasili nchini kutafanyika ibada ya ya mazishi na kutoa fursa ya watanzania kutoa heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Butiama kwa mazishi.

No comments:

Post a Comment