TTCL

EQUITY

Wednesday, October 29, 2014

Msanii wa Kaole awapa somo Bongo Movie

Nora aliwahi kuwika katika kundi la sanaa za kuigiza la Kaole akiwa na Dr. Cheni, Seki na Swebe.

Mkongwe wa sanaa ya maigizo nchini, Nuru Nasoro, maarufu kama ‘Nora’ amesema kusambaratika kwa kundi la Bongo Movie kumewadhalilisha wasanii wakongwe ambao waliweza kuitangaza na kuiheshimu fani hiyo.
Nora, ambaye enzi za uigizaji wake alifanya vyema katika kazi akiwa na kundi la Sanaa la Kaole, alisema kwamba, uroho wa madaraka na chuki baina ya wasanii ndiyo chanzo cha kusambaratika kwa kundi hilo.
Alisema wasanii wa kike nchini kazi yao kubwa kwa sasa imekuwa ni kuuza sura na hawana kipaji kama ilivyokuwa kwao ambako waliiwezesha tasnia hiyo kuheshima.

No comments:

Post a Comment