TTCL

EQUITY

Monday, December 2, 2013

MWALIMU ASIMAMISHWA KAZI BAADA KUTUPIA MTANDAONI PICHA ZA NUSU UCHI

Pictures of teacher Carly McKinney
MWALIMU mmoja amesimamishwa kazi baada ya picha zake za nusu uchi huku zingine akionekana anavuta bangi kunaswa kwenye mtandao wa Twitter.
Carly McKinney, 23 alipigwa picha akiwa anacheza sarakasi (miguu juu mikono chini) huku akiwa na nguo zake za ndani.

Picha zingine zilimuonyesha mwalimu huyo wa hesabu anayefanya kazi Overland High School huko Aurora, Colorado nchini Marekani akionyesha tattoo kwenye tumbo lake akiwa na kichupi.


Picture of Carly McKinney
Baadae Carly alikiri kuwa yeye na rafiki yake walifungua akaunti ya Twitter lakini akisema ilikuwa ni ya mzaha tu na hakujua kama mwenzake alikuwa akizitumia picha zake.
Hata hivyo wanafunzi wamemtetea na kusema mwalimu wao hastahili kuadhibiwa kwa kile alichofanya kwenye muda wake wa nje ya kazi.
Mwanafunzi Shaun alisema: “Ni mwalimu ambaye tofauti ya umri kati yake na miongoni mwa wanafunzi wakubwa ni miaka mitano au sita, kwahiyo tunafanana na mambo yake binafsi”

No comments:

Post a Comment