Kila mwaka Siku ya mwisho ya Mwezi wa Pili huadhimishwa Siku ya ‘Rare Disease’  duniani kote. Kwa mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika leo 29 Februari 2016.
Kwa Tanzania, Sharifa Mbarak ambaye ni mama mwenye watoto wawili ambao waliathirika na magonjwa hayo yasiyotambulika anatarajiwa kuongea na Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakiwamo na madaktari wa watoto  akiwemo Dr. Mariam wa Agakhan na Professor Kareem wa Muhimbili,Monica Joseph pamoja mdau kutoka Philips Medical Systems.
Tukio hilo linatarajiwa kufanyika leo kuanzia saa nne asubuhi, katika hotel ya Serena Dar es Salaam,hivyo unakaribishwa katika kampeni ya kuhamasisha magonjwa yasiyotambulika.
Tunaomba ushiriki wako katika siku hii muhimu kwa Watoto wa Sharifa na watoto wote duniani wanaoteseka na magonjwa haya.