TTCL

EQUITY

Monday, November 18, 2013

WILLIAM MALECELA AMUOMBA RADHI MZEE KAPUYA


Mimi nikiwa Mwana CCM na Kiongozi pia wa CCM ngazi ya Taifa na Blogger, naomba kusimama mbele ya Mheshimiwa Mbunge Kapuya na Taifa zima la Tanzania pamoja na wasomaji wangu wote wa Blog na meble ya Mungu, kukubali makosa na kuomba radhi, kwake na kwa Mungu wangu zaidi. Mimi ni mmoja wa watu wa kwanza kuamini hadithi iliyojitokeza hivi karibuni kwamba Mheshimiwa Kapuya amembaka na kumuambukiza Ukimwi na kutishia kumuua msichana wa miaka 14.

Leo ninaomba kusimama hapa na kusema kwamba hii habari ni uongo na ni uzushi wa hali ya juu sana uliotengeenzwa na msichana mzoefu wa uzushi ambaye kwanza si kweli kwamba ni Mwanafunzi, pili ni Mtumzima mwenye mtoto tayari hata kabla hajakutana na Mh. Kapuya, pia ni muongo na mzushi mzoefu aliyewahi kuwadanganya pamoja na Mkurugenzi wa CRDB Bank, pamoja na kuidanganya TAMWA ambayo iliishia kumuripoti polisi na kuishia kwake kukaa rumande Segerea kwa muda mrefu sana.

Kwa nini niliaiamini hii hadithi ni kwamba kuna siku mimi binafsi tulikuwa tumekaa faragha na Viongozi wengine Watatu wakubwa wa Taifa ambapo mbunge mmoja aliyedai kuijua kwa undani hii hadithi na kuhusiaka nayo, alianza kutuelezea hii hadithi kwa kutmia details kubwa kubwa sana, binafsi nilikuwa ninamuamini sana yule mbunge mpaka leo nilipothibitisha kwa 100% kwamba hii hadithi haiko sawa either na yeye ni muongo wa makusudi mwenye nia mbaya na Mh. Kapuya au na yeye alidanganywa na huyu msichana, ambaye jina lake kamili ni Hamida as opposed na majina mengi ya uongo ambayo amekuwa akiyatumia kudanganyia watu.

Ninaomba kuwa wa kwanza kubeba huu msalaba, najua kwamba sio rahisi kueleweka na wengi ambao tulishamuhukumu Mh. Kapuya, lakini ukweli ni kwamba ni hadithi ya kutunga iliyoutngwa na msichana mmoja aliyebobea katika uzushi na uongo wa hali ya juu sana. Majuzi Waziri mmoja ninayemuamini sana katika Serikali ya sasa alinishitua kwamba hii hadithi ni ya uongo niiifuatilie tena, lakini sikuamuamini mpaka leo asubuhi sana nilipopigia sim na gazeti moja maarufu sana la Udaku, walioniambia kwamba hii habari si ya kweli na kwamba wanaye huyu msichana pale ofisini kwao, toka asubuhi mpaka sasa nimekuwa kwenye uhakiki wa hii ishu, na sasa ninasema wazi na tena kwamba:-

NINAMUOMBA RADHI SANA MH. KAPUYA NA NI MATUMAINI YANGU MAKUBWA SANA KWAMBA WALE WOTE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU TUTAKUBALI MAPUNGUFU YETU KAMA WANADAMU NA KUMUUNGAMIA CHINI MUNGU WETU, NI KWELI MH. KAPUYA ALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HUYU BINTI LAKINI YA HIARI SIO KAMA ILIYOELEZWA NA SI KWELI KWAMBA HUYU BINTI NI MWANAFUNZI, HAPANA ANA MTOTO TAYARI NA PIA ALISHAWAHI KULIDANGANYA JESHI LA POLISI HUKO NYUMA.

Wale wote tunahusika na media tujifunze tena na hili fundisho, tujitahidi kuwa waadilifu na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruka na hadithi nzito kama hii ambayo inaweza kummaliza mwananchi mwenzetu, au kiongozi bila sababu za msingi wala ukweli.

AGAIN NI MATUMAINI YANGU KWAMBA WALE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU MHESHIMIWA KAPUYA, TUTAJITOKEZA TENA IN THE PUBLIC NA KUMUOMBA RADHI NA MSAMAHA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!

WILLIAM MALECELA

Kutoka majid mjengwa blog;

TENA MZEE ALIKOROGA;DUU

SIKU chache baada ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa utetezi wa kujikanganya.

Akizungumza kupitia kwa wakili wake, Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.(HD)

Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.

Hata hivyo, katika namna ya kushangaza, Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.

Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo, Novemba 9, mwaka huu, gazeti hili liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi sita iliyopita.

Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.

Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.

Utetezi wake pia unaongeza utata kwani hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.

Katika utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.

Alilishutumu gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye tasnia ya habari.

Hata hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.

Hata alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.

Lakini muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo iliita bila kupokelewa.

Wakili Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.

"Kwa sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima, mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo atavishitaki mahakamani.

"Kama hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi," alisema.

Aliongeza kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.

Memba aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima haiusiani na chama chake wala serikali.

Kwa siku mbili mfululizo gazeti hili lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.

Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Prof. Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.

Juzi alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: "Chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"

Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu."

Baadhi ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia watoto hao, ambao ni yatima.

Mtoto huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.

Hata hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.

Juzi gazeti hili lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili.CHANZO TANZANIA DAIMA.

MAONI YA ASENGA;

HILI SUALA LINAMHUSU MBUNGE,TENA WA CHAMA MAKINI CHAMA CHANGU,KAMATI YA BUNGE ICHUNGUZE NA SPIKA AJE MBELE YA UMMA KUWEKA WAZI UKWELI,,,KAMA AMBAVYO ATAKUJA WAZI KUHUSU SUALA LA LEMA

No comments:

Post a Comment