RAIS wa Malawi, Joyce Banda ametajwa
kuendeleza chokochoko baina ya nchi yake na Tanzania, huku sasa
akidaiwa kutumia redio na runinga za nchini mwake kutangaza kuwa mkoa wa
Ruvuma, viongozi na wananchi wa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake.
Aidha,
amesitisha safari za meli ya mv Ilala iliyokuwa ikifanya safari kwenye
Ziwa Nyasa kusafirisha mazao na wananchi wa ukanda huo upande wa
Tanzania.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa soka wa
Mbambabay jana, Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba, alisema Rais
Banda ambaye aliibua upya mzozo wa mpaka baina ya nchi hizi mbili, kuwa
ni mkorofi kutokana na kufanya vitendo vinavyoonesha uhusiano baina ya
nchi hizi mbili kuzorota.
Komba alibainisha vitendo hivyo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, akisema imefika mahali Rais Banda anapotosha ukweli
kuhusu mpaka kati ya nchi hizo mbili na kudai sehemu ya mwambao wa Ziwa
upande wa Tanzania ni yake.
Mbunge
huyo alisema jimbo la Mbinga Magharibi ambalo ni Wilaya ya Nyasa,
wanasikiliza matangazo ya redio za Malawi, na anazitumia kupotosha umma
kuwa ukanda wa Ziwa Nyasa ni mali yake na wananchi wanaamini hivyo.
Rais
Banda anatangaza kupitia vyombo vya habari vya nchi yake ambavyo
vinasikika vizuri katika wilaya hiyo kutokana na wilaya ya Nyasa
kutopata mawasiliano ya redio na runinga za nchini.
Komba alisema kutokana na wilaya hiyo kukosa mawasiliano ya vyombo vya habari, wananchi wake wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba za viongozi wa Taifa.
Komba alisema kutokana na wilaya hiyo kukosa mawasiliano ya vyombo vya habari, wananchi wake wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba za viongozi wa Taifa.
Wananchi
wanakosa kusikiliza matangazo zikiwamo hotuba ya Rais Kikwete ya kila
mwezi na hotuba za viongozi wengine wa kitaifa wakiwamo Makamu wa Rais
na Waziri Mkuu.
“Kutokana
na kukosekana usikivu huo, Rais Banda anatumia nafasi hiyo kutangaza
kuwa viongozi wote wa wilaya na mkoa na eneo lote ni mali yake,” alisisitiza Komba.
Aliongeza kwamba watu wote walioko kwenye mkutano huo isipokuwa Katibu Mkuu Kinana, akiwamo Dk Asha-Rose Migiro ambaye alizaliwa Mbambabay wote ni mali ya Rais Banda.
Aliongeza kwamba watu wote walioko kwenye mkutano huo isipokuwa Katibu Mkuu Kinana, akiwamo Dk Asha-Rose Migiro ambaye alizaliwa Mbambabay wote ni mali ya Rais Banda.
Mbunge
huyo alisema wananchi wa eneo hili nao ni Watanzania wanaostahili
kusikia na kupata habari za nchi yao, badala ya kusikiliza nyimbo na
matangazo ya Malawi ambayo yanakuwa na ajenda zake.
Mbunge
Komba alimwomba Katibu Mkuu Kinana kwenda kuhimiza kutekelezwa haraka
kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuleta meli ili kuwa na usafiri wa
uhakika wa mali na wananchi katika eneo hilo.
Kinana
alisema ahadi ya meli ya Rais, hiyo ana uhakika itatekelezwa na
kufafanua kuwa meli tatu zinatengenezwa Korea Kusini na zitakapokamilika
ya Ziwa Nyasa itapelekwa kutoa huduma.
Alisema
baada ya Banda kuondoa meli hiyo wananchi wa Mbambabay wanatumia boti
dogo kusafirisha abiria na mizigo, hali ambayo inatia shaka.
Kinana
alisema amesikia kilio cha Mbunge Komba, kwamba ahadi ya Kikwete
itatekelezwa ili kuwapa wananchi usafiri wa meli, ingawa itatumia muda
kutokana na kuhitaji muda mwingi kubuni na kutengeneza.
Credit: HABARI LEO
No comments:
Post a Comment