PROF Juma Kapuya MB (CCM) Urambo Magharibi |
HATIMAYE
binti anayedaiwa kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma
Kapuya (CCM), amefungua jalada Polisi dhidi ya mbunge huyo.
Habari
za kipolisi ambazo Tanzania Dama limezipata, zinasema kuwa binti huyo
ambaye anadai kubakwa na kisha kutishiwa kuuawa na Profesa Kapuya,
amefungua jalada namba OB/RB/21124/13katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Harakati
za kufungua jalada hilo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana
ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa
kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.
Akiwa kituoni hapo, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake
na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke
malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikiri polisi kufungua
jalada hilo na kuongeza kwamba hivi sasa wanafanya uchunguzi kubaini
kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa
maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
“Tumefungua
jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika
na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.
Habari
zaidi zinasema polisi wamechukua namba ya Kapuya inayodaiwa kutumika
mara kwa mara kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa binti huyo, akitishiwa
kuuawa.
Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa
kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya
kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya
mtandao kwenda kwa binti huyo.
Moja ya ujumbe wa vitisho unaodaiwa kutumwa na Kapuya kupitia simu hiyo unasomeka hivi;
“Mkiuawa
itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na
serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo
gazeti ni Mbowe sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela
leo? Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua
lazima niwaue wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si
wamekuficha tuone utalindwa milele maana washatengeneza hela, lazima
mvae sanda tu hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia
watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana
nasi.”
Pia simu hiyo iliwahi kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaosomeka hivi;
“Ni
lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Sitta
asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi? We
unadhani nani atakaenifunga, ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache
mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone.”
Mbali
na kutishia kumuua binti huyo na ndugu yake na mtu mwingine yeyote
atakayejitokeza kumsaidia, Tanzania Daima limenasa baadhi ya mawasilino
ya simu za ujumbe mfupi wa kuhamisha fedha kutoka kwa Profesa Kapuya
kwenda kwa binti huyo ambaye mbunge huyo alikana kumfahamu na kwamba
hajawahi kukutana naye.
Tanzania Daima pia lilinasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda kwa binti huyo.
Baadhi
ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu
kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo
kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya
matunzo.
Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: U26UG365 Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe31/8/13 saa 3:28 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000
V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000 kutoka kwaJUMA KAPUYA Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040.
R93NY448 Imethibitishwa Umepokea Tsh 505,000 kutoka kwaJUMA KAPUYA Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000.
Kutokana
na mfululizo wa habari hiyo, Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake
Yasin Memba, ametishia kuliburuza mahakamani Tanzania Daima endapo
halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.
CREDIT: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment