TTCL

EQUITY

Thursday, November 28, 2013

Magazeti ya Udaku yazidi kumwandama Bob Junior, yadai kuwa ana uhusiano na Vanessa Mdee.

 Magazeti ya Udaku yazidi kumwandama Bob Junior, yadai kuwa ana uhusiano na Vanessa Mdee
Mwanamuziki wa kizazi kipya Bob Junior
Magazeti ya udaku yameendelea kumnyima raha na usingizi Rais wa Masharobaro, Bob Junior na leo yamemuangushia bomu jingine. 

Gazeti la Sani leo limeibuka na habari yenye kichwa cha habari, ‘Baada ya ndoa yake kuvunjika: Bob Junior aibuka kwa Vanessa Mdee.  

Habari hiyo imeonesha kumkera msanii huyo aliyemshirikisa Vanessa kwenye wimbo wake ‘Bashasha’ na kuamua kuandika kwenye Facebook, “hichi ndicho walitaka kusema ,haya msha sema kingine kipi????’


Awali gazeti jingine la udaku liliandika habari kuwa Bob Junior huvaa nguo za ndani za kike ambazo kabla ya hapo zilidaiwa kuwa za mwanamke wa nje na kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake.

No comments:

Post a Comment