TTCL

EQUITY

Monday, November 18, 2013

FAIDA YA POMBE FEDHEHA, MWANADADA AFUNGUA SHOO BILA KIINGILIO KWAKUTEMBEZA CHUCHU ZAKE HADHARANI

 Mrembo wa haja ambaye jina halikupatikana mara moja, amenaswa akiwa matiti  nje baada ya kulewa mchana kweupe na kulizwa mkoba wake kisha kuzua varangati zito,
Varangati hilo lililonaswa na kachero wetu lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Sinza- Afrika Sana jijini Dar.
 
Katika sinema hiyo ya bure, mrembo huyo alishuhudiwa akipigana na kila mtu aliyekutana naye mbele yake huku akivua nguo kuashiria kuwa ‘pombe si chai’.

Kuna wakati mwanadada huyo alikatiza barabarani bila kujali magari na nusura agongwe jambo lililosababisha mtafaruku wa foleni huku mwenyewe akidondoka kama ‘embe dodo’ lililoiva.


Baada ya timbwili hilo kuchukua takriban dakika 35, ilibidi wasamaria wema kuingilia kati na kumshika huku akiwapiga baada ya kuona huenda angeumizwa.
Baadaye watu hao walifanikiwa kumtoa eneo la barabara huku wakimsitiri kwa kupandisha nguo kufunika nido kisha kumpeleka pembeni na kumtuliza.
 
“Kweli pombe siyo chai. Yaani msichana mzuri lakini ona alivyojidhalilisha,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.

No comments:

Post a Comment