Mpendwa,
Siku
moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga
kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini
cha kufanya. Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia
kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya
kumtoa.
Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote
wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani
ya kisima. Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwakinatokea
akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda
aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho
kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo
la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya
kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku
akipiga hatua moja kuja juu.
Kadri mkulima na majirani
walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi
kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae,
kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na
kuja juu.
FUNZO:
Maisha
yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji
kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la
kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya
kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila
kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua
hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.
2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.
3.Tosheka / rizika na ulichonacho.
4. Toa zaidi.
5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.
MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KILA JAMBO....
No comments:
Post a Comment