TTCL

EQUITY

Friday, July 5, 2013

YALIYOJIRI DUNIANI WIKI HII

Todd Saunders akiwa na Kapteni wa Jeshi la Marekani, Micahel Potovzniak, ambaye wamekuwa wapenzi kw a muda wa miaka kumi, wakifurahi baada ya kusaini cheti cha ndoa yao, ambapo sasa wamerasimishwa baada ya hukumu ya hivi karibuni ya mahakama ya juu kwenye jimbo la California. ©Stephen Lam/Reuters
Grace Meier, kulia akimtazama mama yake, Sallee Taylor katikati na  mpenzi wake, Andrea Taylor wakati wa sherehe ya harusi iliyofanyika West Hollywood, California, Julai Mosi. Jiji la West Hollywood limetoa ofa ya kufungisha ndoa za jinsia moja bure kwa wanaotaka kila Jumatatu.
Mashabiki wa kutoa mimba wakiwa katikati ya duara, wakati wanaopinga ndoa hizo wakizunguka duara lao huku wakipingana nao kuhusu muswada unaotarajiwa kusikilizwa kwenye jimbo la Texas. Gavana wa jimbo hilo, Rick Perry amewaita watunga sheria kukutana kwa ajili ya kikao kingine huku ajenda kubwa ikiwa ni suala hilo.
Mpita njia kando ya shule iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi eneo la Blang Mancung, Aceh, Indonesia mnamo siku ya Alhamisi tarehe 4 Julai. Watu 30 wanakadiriwa kufa kwenye tetemeko hilo, polisi na wanajeshi wanafanya jitihada kusaka watu wengine 12 wanaoaminika kupotea. 
Pamela Knox (60) wa Toledo, akiwa amedumbukia kwenye shimo ambalo limesababishwa na kuharibika kwa njia ya maji chini kwa chini jimboni Ohio siku ya Jumatano Julai 3. Bibi huyo alipelekwa hosptialini licha ya kutoumia kwenye ajali hiyo. 
Wapinzani wa aliyekuwa Rais wa Misri, Mohamed Mosri wakishangilia kwenye uwanja wa Tahrir Square siku ya Jumatano mara baada ya kiongozi huyo kuondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo Jumatano tarehe 3 Julai.
Mchezaji baseball wa Arizona Diamondbacks akiwa bize kwenye harakati za kuitafutia ushindi timu yake dhidi ya Atlanta Braves Juni 29 huko Atlanta.
Marais Obama na Kikwete wakicheza kufuata mdundo wa muziki wa kiasili wakati Rais Obama alipotua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment