HATIMAYE MKOA WA MBEYA WAGAWANYIKA WAZALIWA MKOA MWINGINE WA SONGWE
MKUU WA MKOA WA MBEYA
ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC) JIJINI MBEYA
KATIBU TAWALA WA MKOA
MARIAM MUTUNGUJA AKISOMA TAARIFA YA MKUTANO
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA
MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO
MBUNGE WA MBOZI MASHARIKI
NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MBEYA GODFREY ZAMBI AKICHANGIA JAMBO KATIKA KIKAO
HICHO
MKUU WA WILAYA WA MBEYA
DR. NORMAN SIGARA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO
MBUNGE WA VITI
MAALUMU(CCM) MKOA WA MBEYA DR. MARY MWANJELWA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO
HUO
MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS
kAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
MKUU WA WILAYA YA
RUNGWE CRISPIN MEELA AKIZUNGUMZA JAMBO
WAJUMBE WAKIWA
WANAFUATILIA MKUTANO HUO
Songwe ndilo jina
lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao
utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa
huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.
Mkoa wa zamani Mkoa wa
Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu
yatabaki pale pale Jijini Mbeya.
Kupatikana kwa jina hilo na
mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika leo
katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro.
Jina la Mkoa huo Mpya
limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe
ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.
Hata hivyo kuhalalishwa kwa
jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya
RCC.
No comments:
Post a Comment