TTCL

EQUITY

Tuesday, July 2, 2013

MAMA MICHELLE OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE

1 

Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA  jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo, Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako  katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana  na watoto wao jioni hii Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE 2 
Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii. 3 
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi. 4 
Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete  6 
Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama 7 8 9 
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii 10 
Makachero wa Marekani wakiwa kazini  11 
Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wake wa Viongozi wakati alipowasili katika ofisi za WAMA tayari kwa kumpokea mgeni wake Mama Michelle Obama

No comments:

Post a Comment