TTCL

EQUITY

Tuesday, July 2, 2013

SPIKA WA BUNGE LA OMAN NA UJUMBE WAKE ATEMBELEA HIFADHI YA SERENGETI KWA MAPUMZIKO YA MWISHO WA WIKI


1   
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali (kulia) akiongea na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti muda mfupi baada ya kupokelewa katika Uwanja wa Seronera alipowasili kwa mapumziko mafupi. Katikati ni Afisa Mwandamizi wa Bunge Said Yakub.PICHA NA PASCAL  SHELUTETE WA TANAPA 2 
Msafara wa Spika wa Bunge la Oman ukishuhudia sehemu ndogo ya msafara maarufu wa Nyumbu “ Great Migration” katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. 3 
Simba akiwa amejipumzikia Hifadhi ya Serengeti na kuwa kivutio kizuri kwa msafara wa Spika wa Oman na ujumbe wake. 5  
 Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali (kushoto) akihojiwa na Mwanahabari juu ya kilichomvutia ambapo hakusita kusema kuwa Serengeti ni zawadi ya Watanzania tunayopaswa kuitunza kwa faida yetu. 6 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. Abdulkarim Shah (kushoto) ambaye alikuwa miongoni mwa msafara wa Spika wa Oman akihojiwa na wanahabari ndani ya Hifadhi ya Serengeti. 7   
Picha ya pamoja ya baadhi ya Wabunge wa Bunge la Oman na wenyeji wao Tanzania katika Hifadhi ya Serengeti.
 8Wanahabari walio katika msafara wa Spika wa Oman wakipiga picha na Afisa Habari wa Bunge la Oman Said Al Marjibi (wa nne kushoto)

No comments:

Post a Comment