Arusha, Tanzania
MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini
Godbles Lema ameachiwa kwa dhamana mpaka tarehe 29 mwezi wa tano kesi
hiyo itakaposikilizwa tena katika Mahakamana hiyo.
Baada ya Mbunge huyo kuachiliwa
huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana katika Mahakama
hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za Chama hicho
zilizopo maeneo ya Ngarenaro.
Mbunge huyo amekutwa na makosa matatu ambapo kosa la kwanza ni
kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa
‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa
jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa.
Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa "Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya
Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia
kama vile anaingia kwenye send-off.
Kosa la tatu ni pale alipotamka kwa wanafunzi kuwa "Mimi Mbunge wenu
nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa
hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza
hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya
msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo
niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na
kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao
msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’.
No comments:
Post a Comment