MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemnusuru aliyekuwa Mtangazaji
wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Murro na wenzake wawili
katika hatari ya kesi yao kusikilizwa umpya, badala yake itaendelea
kusikilizwa kama rufaa.
Awali kesi hiyo ilikuwa kwenye hatari ya kusikilizwa upya baada ya
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, kudaiwa kufanya makosa katika utoaji
wa hukumu ya Muro na wenzake wawili, Edmund Kapama maarufu kama ‘Dokta’
na Deogratius Mugassa.
Hata hivyo leo Majaji wa Makahama ya rufaa wametupilia hoja za
mawakili wa Serikali waliotoa hoja za kutaka kesi hiyo isikilizwe upya.
Hoja za Jamhuri wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Oktoba 18,
mwaka huu, Mawakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya na Awamu Mbangwa,
waliiomba mahakama hiyo iamuru kesi hiyo isikilizwe upya chini ya
kifungu cha 388 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).
Wakili Mbangwa alidai kuwa Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo (Gabriel Mirumbe) alikosea kisheria katika kuweka kumbukumbu za
mwenendo wa kesi.
mwenendo wa kesi.
Alidai kuwa kutokana na dosari hizo, hata hakimu aliyeandika hukumu
ya kesi hiyo (Frank Moshi) aliegemea katika mwenendo huo ambao
haukurekodiwa vizuri na matokeo yake alitoa hukumu isiyo sahihi.
Wakili Mbangwa alifafanua kuwa katika mwenendo wa kesi hiyo kuna
sehemu za ushahidi wa baadhi ya mashahidi wa upande wa mashtaka,
umerekodiwa kwa namna ambayo hauakisi uhalisia wa kile mashahidi hao
walichokiziunguza. Aliongeza kuwa kuna
baadhi ya sehemu za ushahidi hazikurekodiwa kabisa ikiwemo uamuzi wa
mahakama kukataa kupokea kitabu cha wageni waliokuwa wakifika katika
hoteli ya Sea Clif ambako Muro na wenzake walidaiwa kukutana na Wage.
Pia
alitoa mfano wa maelezo ya onyo ya mjibu rufaa wa kwanza, Muro,
kutokuoneshwa kwenye kumbukumbu kuwa yaliopokewa mahakamani hapo. Majibu
ya utetezi Wakijibu hoja hizo, mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza
na Majura Magafu walidai kuwa malalamiko ya Jamhuri katika hukumu hiyo
hayako wazi na kwamba hata kama yapo lakini hawajaonesha jinsi
yalivyoathiri hukumu hiyo.
Alidai kuwa
kutokuwepo kwa uamuzi wa suala hilo katika kumbukumbu kuliinyima
nafasi jamhuri kujua sababu za kukataliwa kwa kielelezo hico.
Wakili Magafu alidai kuwa mazingira ya kesi walizozitumia Jamhuri ni
tofauti na mazingira ya rufaa hiyo na kwamba kitendo cha Jamhuri kuomba
kesi hiyo isikilizwe upya ni sawa na biashara ya kuchagua mahakimu
kwamba wakishindwa kwa hakimu mmoja wanakwenda kubahatisha kwa hakimu
mwingine. Hata hivyo Wakili wa
Serikari Tibabyekomya alidai kuwa hukumu hutokana na ushahidi wa pande
zote na kwamba kutokurekodiwa vizuri kwa mwenendo huo na kasoro hizo
zilisababisha haki isitendeke kwa pande zote.
Jaji Twaib Jaji Dk Twaib alihoji Jamhuri kama kama mwenendo huo
uliochapwa ndivyo ulivyo kwenye mwenendo halisi. Ili kujiridhisha,
aliamua kusoma mwenendo halisi uliondikwa kwa mkono, lakini yeye binafsi
na hata wakili wa utetezi, Magufu, waalishindwa kuelewa baadhi ya
maneno yaliyoandikwa. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote Jaji Dk Twaib aliahirisha rufaa hiyo hadi leo kwa ajili ya uamuzi. Muro
na wenzake walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 5, mwaka
2010, na kusomewa mashtaka kula njama na kuomba rushwa kutoka kwa
aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage.
No comments:
Post a Comment