Aina mpya ya viini sugu vinavyosababisha Malaria na ambavyo havisikii dawa vimegunduliwa na wanasayansi.
Watafiti wamevigundua viini hivyo Magharibi mwa
Cambodia na wanasema kuwa vina umbo tofauti la genetiki ikilinganishwa
na viini vingine duniani.
Viini hivi ni sugu kiasi cha kutosikia dawa aina ya Artemisinin, dawa yenye nguvu zaidi katika kutibu Malaria.
Taarifa ya kwanza kuwa wagonjwa walikuwa
hawatibiki na dawa hiyo ilitokea mwaka 2008. Tatizo hilo tangu hapo
limeenea katika maeneo mengine ya Asia ya Kusini.
Utafiti huu umechapishwa katika jarida la ''Nature Genetics.''
Mtafiti mkuu Daktari Olivo Miotto, wa chuo kikuu
cha Oxford na kile cha Mahidol nchini Thailand,amesema kuwa dawa zote
zenye uwezo wa kuua Malaria na ambazo zimevumbuliwa katika miaka ya hivi
karibuni, zimekuwa ovyo katika kutibu Malaria.
"Dawa ya Artemisinin kwa sasa inafanya kazi
vyema. Ndio silaha nzuri zaidi dhidi ya ugonjwa huo na tunahitaji
kuendelea kuitumia,'' alisema Daktari Miotto
Magharibi mwa Cambodia kumetajwa kama sehemu yenye Malaria sugu.
Haileweki ni kwa nini tangu mapema miaka ya
1950, viini vya Malaria katika eneo hilo, vimekuwa sugu. Tatizo hilo pia
limesambaa hadi katika sehemu kadhaa za Asia na Afrika.
Kwa sasa wanasayansi wana wasiwasi kuwa hali
sawa na hiyo itajitokeza kwa dawa ya Artemisinin. Dawa hiyo inatumika
kote duniani kukabiliana na Malaria, na inaweza kutibu ugonjwa kwa siku
chache tu ikiwa itatumika na mchanganyiko wa dawa zengine.
No comments:
Post a Comment