TTCL

EQUITY

Wednesday, November 28, 2012

Maswali yanayo ulizwa na wengi

Mshiriki wa kipindi cha Sema Kenya

Ni nyadhifa zipi za kugombewa katika uchaguzi mkuu ujao?
Kuna nyadhifa sita za kugombewa wakati wa uchaguzi kwa mujibu wa katiba. Nazo ni:
• Rais
• Mwanachama wa Bunge la Kitaifa (Mbunge).
• Mwanachama wa Seneti ( Seneta).
• Gavana
• Mwakilishi wa wanawake.
• Mwakilishi wa serikali ya Kaunti.

Bunge litakuwa na muundo gani?
Bunge litakuwa na:
• Bunge la Kitaifa
• Seneti.

Uanachama wa Bunge la Kitaifa ni upi?
Bunge la kitaifa litakuwa na :
• Wanachama mia mbili tisini (290) waliochaguliwa na wapiga kura kutoka kila eneo bunge.
• Wanawake arobaini na saba (47) waliochaguliwa na wapiga kura kutoka kila kaunti.
• Wanachama kumi na mbili ( 12) walioteuliwa na vyama vya kisiasa vya bunge kulingana na usawa wa wanachama wa bunge la kitaifa, kuwasilisha maslahi maalum ya watu wakiwemo vijana, walemavu na wafanyikazi.
• Spika ambaye ni mwanachama maalumu.

Ni nani wanachama wa Seneti?
• Bunge la Seneti ina wanachama arobaini na saba (47) waliochaguliwa na wapiga kura kutoka kila kaunti.
• Wanawake kumi na sita (16) walioteuliwa na vyama vya kisiasa kwa mujibu wa idadi ya wanachama arobaini na saba (47) waliochaguliwa katika seneti.
• Mwanaume na mwanamke anayewakilisha vijana.
• Mwanamme na mwanamke anayewakilisha walemavu.
• Spika ambaye ni mwanachama maalum.

Je nini tofauti baina ya Bunge la Kitafa na Seneti ukizingatia majukumu yake?
• Bunge la Kitaifa linawasilisha raia na maslahi ya maeneo bunge ilhali bunge la Seneti linawasilisha maslahi ya kaunti na serikali zake.
• Bunge la Kitaifa lina tunga sheria za nchi ilhali ile ya seneti za kaunti peke yake.
• Bunge la Kitaifa linaamua ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya serikali ya kitaifa nay a kaunti ilhali ile ya seneti inaamua ugavi wa mapato ya kitaifa miongoni mwa kaunti.
• Japo mabune yaote mawili yata husika na kuchunguza utenda kazi wa rais, naibu rais na maafisa wengine wa serikali ni bunge la Kitaiffa pekee kitakachokuwa na mamlaka ya kuanzisha utaratibu wa kuwaondoa kutoka mamlakani, huku seneti ikitoa maamuzi tu kuhusu hoja hizo.

Serikali ya kaunti ni ipi na nani wanachama wake?
Hii ni serikali iliyoundwa katika kila kaunti kwa minajili ya kutawala na kuendesha shughuli za kauti.
Serikali ya kaunti inajumuisha:
• Bunge la Kaunti
• Kamati tendaji ya kaunti.

Wanachama wa bunge la kaunti ni:
• Mwakilishi wa wadi.
• Wanachama wa viti maalum kuhakikisha kwamba hakuna kuzidi kwa thuluthi mbili za jinsia moja ya wanachama kutoka kwa orodha ya vyama vya kisiasa.
• Wanachama wa makundi yaliyotengwa wakijumuisha walemavu na viajana ambao wataamuliwa na bunge kutoka orodha iliyowasilishwa na vyama vya kisiasa vinavyowakilishwa katika bunge la Kaunti.
• Spika ambaye ni mwanachama maalum.

Ni nani wanachama wa kamati tendeji za serikali ya Kaunti?
• Gavana wa Kaunti pamoja na makamu wake.
• Wanachama walioteuliwa na Gavana wa Kaunti kwa makubaliano na bunge la kaunti ambao si wanachama wawakilishi wa bunge hilo.

Ni yapi majukumu ya kamati tendaji za kaunti?
• Kutekeleza sheria za kaunti.
• Kutekeleza sheria za kaunti katika kaunti.
• Kuendesha na kuratibu majukumu ya utawala wa kaunti pamoja na idara zake.
• Kundaa sheria zilizopendekezwa ili zizingatiwe na bunge la Kaunti.
• Kutoa ripoti za mara kwa mara katika bunge la kaunti kuhusu maswala yanayohusu kaunti.

No comments:

Post a Comment