Mkurugenzi
Msaidizi wa Habari, elimu na mawasiliano wa bodi ya mikopo Tanzania,
Cosmas Mwaisobwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
leo wakati wa tukio hilo la juu ya tathimini ya notisi ya siku 60
kumalizika na kuongeza siku zingine 30, zinazoanzia leo Mei 20. wengine
ni viongozi wa bodi hiyo akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo
Bw. Robert Kibona na Meneja wa Habari , Elimu na Mawasiliano Bw. Omega
Ngole (kulia). Wengine ni wanahabari wakifuatilia tukio hilo.
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeamua kuongeza siku
Thelathini (30) ilikutoa fursa kwa wanuifa na waajiri waliobaki
kujitokeza kulipia madeni yao waliokopa kupitia bodi hiyo, kuanzia 1994
hadi hivi sasa.
Wakizungumza
na waandshi wa Habari mapema leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Msaidizi Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bw.
Robert Kibona alisema kuwa tathimini ya agizo la siku 60 kwa wadaiwa na
waajiri limekwisha na wamejitokeza wa wingi licha ya kuwapo na wengine
walioomba kuongezewa muda kwa siku za kufanya hivyo ilikuweza
kujitokeza.
“Machi
14 mwaka huu tulitoa notisi ya siku 60 kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu
ta juu kujitokeza na kuanza kurejesha na Mei 13, 2016 siku hizo sitini
(60) zilikamilika.
Wadau
watatu muhimu ambao Bodi inawatambua kutokana na sharia ya Bodi ya
(SURA 178) ni pamoja na Mnufaika, Mwajiri na Mdhamini mbao kisheria
wanatakiwa kurejesha mikopo hiyo baada ya miezi 12 tu ya mnufaika
kumaliza elimu yake, hivyo mwitiko kwa wanufaika na waajiri ulikuwa ni
mkubwa kwa kujitokeza kujua madeni yao na kulipa” alisema Bw Kibona.
Wanufaika
2,007 ambao wanadaiwa jumla ya Tsh 1.93 Bilioni waliwasiliana na bodi
ya Mikopo kwa njia mbalimbali ikiwemo kufika katika ofisi hizo. Pia
waajiri 1528 waliweza kuwasilisha taarifa za wanufaika 19,714 ambao
wanadaiwa Tsh 149.5 Bilioni. Hata hivyo jumla ya Wanufaika 21,721 ambao
wanadaiwa jumla ya Tsh 151,5 Bilioni ambapo kati ya fedha hizo, kila
mwezi wanatarajia kukusanya Tsh, 1.8 Bilioni na hivyo kuongeza kiasi
cha ukusanyaji kwa mwezi kufikia Tsh.8.0 Bilioni ifikapo mwezi Juni
2016.
Hata
hivyo Bw. Kibona ameongeza kuwa, baada ya mwitiko kuwa mkubwa hivyo
wameamua kuongeza siku hizo 30, ambapo baada ya hapo watachukua hatua
kali za kisheria kwa wahusika wote waliooanishwa katika SURA ya 178.
No comments:
Post a Comment