Na Ally Daud – Maelezo
Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama vinazidi kupungua kutoka siku hadi siku katika kufikia malengo ya milenia .
Akizungumza
hayo katika hafla fupi ya kuzindua maonesho ya picha Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto ,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando amesema kuwa Tanzania imepiga
hatua katika kufikia malengo ya milenia kwa kupunguza Idadi ya vifo kwa
watoto wachanga na wakina mama.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke kulia akikata utepe kuashilia kuanza
rasmi kwa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya Taifa mpaka Juni
10 mwaka huu jijini Dar es salaam na wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando.
“Tumefanikiwa
kupunguza Idadi ya vifo kwa watoto wachanga na wakina mama ili kufikia
malengo ya milenia kwa upande wa afya kupitia mfumo wa kujiunga na bima
ya afya kwa jamii,” alisema Dkt. Mbando.
Mbali
na hayo Dkt. Mbando amesema kuwa amewakaribisha wananchi wote hususani
wakazi wa Dar es salaam kuudhuria maonesho hayo yaliyofunguliwa leo
yenye kauli mbiu ya “Huduma Bora kwa Afya Bora” yatayofikia kilele mpaka
Juni 10 mwaka huu ili kupata ujumbe zaidi kupitia picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa jijini.
Aidha
ameipongeza Serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake kwa kushirikiana
vizuri na Serikali ya Tanzania na kukubaliana kupata msaada wa Euro
Milioni 47 kwa muda wa miaka mitatu ijayo katika kuinua sekta ya Afya.
Kwa
upande wa balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke amesema kuwa mchango
wa Serikali ya ujerumani kwa sekta ya afya Tanzania utaendelea kuwa
sehemu ya mpango wa ushirikiano wa nchi mbili ili kuinua sekta hiyo
nchini.
Balozi
wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke akiongea na waandishi wa habari na
Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH) hawapo
pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho
ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi
wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii , Jinsia na Watoto,
Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando akiongea na waandishi wa habari
na Wadau wa Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH)
hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika
Makumbusho ya Taifa mpaka Juni 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Mshauri
wa ufundi kutoka Mpango wa Tanzania na Ujerumani kusaidia Afya (TGPSH),
Dkt. Baltazar Ngoli wa kwanza kulia akitoa maelekezo ya picha kwa
Balozi wa Ujerumani Mhe. Egon Kochanke wa pili kulia pamoja na
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Margaret Mbando wa tatu kulia
wakati wa ufunguzi wa maonesho ya picha yanayofanyika Makumbusho ya
Taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment