1. Mara kwa mara wanakuza wigo wa maono yao.
Mbali na ile ndoto waliyokuwa nayo huchukua fursa kwa ukuaji wa uchumi, ukosefu wa huduma na teknolojia kufungua fursa mbalimbali. Mwenda kwao hafungwi mlala.
2. Ni watu ambao hufanya kazi kwa malengo.
Hutafuta muda mzuri wa kukaa chini na kutathmini malengo yao, kujikosea pale walipokosea kisha kuandika mpangokazi wa kuufuata ndani ya muda fulani ili kukuza biashara au huduma husika.
3. Wanachukua Hatua
Watu hawa wanaelewa kuwa wasipofanya kazi basi ni ngumu kwa wao kufanikiwa. Hawalalamiki bali hufanya waliwezalo kufanikisha malengo waliyojiwekea.
4. Hujiweka karibu na wenye manufaa kwao.
Ndugu yangu, Bahari haivukwi kwa kuogelea.
5. Ni wanafunzi maisha yote.
Mara kwa mara hutafuta njia mbalimbali za kujifunza na kujiendeleza kupitia maisha ya kila siku, toka kwa watu wanaokutana nao na mafunzo ambayo yanatolewa na Mwalimu Dunia smile emotico"Chuma hakimegwi - changarawe haitafunwi."
6. Huwatumikia wengine.
Wanaelewa kuwa mafanikio ya biashara au huduma yoyote ni katika kusaidia watu na kutatua matatizo yao. Hivyo huweka akili zao katika kuhakikisha wanachofanya kinagusa na kubadilisha maisha ya watu. Hufanya kazi kwa akili kwamba wao ni watumwa kwa wateja. Kumbuka kuwa Mti haushuliki ila kwa mti mwingine.
7. Wanafanya kazi kuliko wengine.
Kuna msemo unaosema “Jitihadi haiondoi kuduru ya Mungu.” Watu wengi hudhani kuwa waliofanikiwa kibiashara ni watu wenye bahati lakini ukweli ni kwamba hufanya kazi sana Zaidi ya muda wa kawaida, hujitoa na kuvuka mipaka ili kufanikisha mambo waliyojiwekea hata kama hawana fedha.
8. Huhifadhi chochote kwa Manufaa ya baadae.
Watu hawa hutambua kuwa changamoto ni kwa binadamu hivyo hujipanga kwa kuweka kiasi kidogo kwa ajili ya baadae kiafya na kimaisha. Ndio maana nchi za wenzetu wanathamini huduma kama zinazotolewa na mfuko wa jamii, PSPF Tanzania Jua kwamba Mfinyanzi hupika kwa vigae.
9. Hawakubali kushindwa kuwafanye wasifike mbali.
Wakati wengine wanakata tamaa pale wanaposhindwa wao wana#InukaEndelea na kujaribu vitu vipya. Wanaelewa kuwa mafanikio huhitaji majaribio na katika majaribio zimefichwa changamoto mbalimbali. Usisahau kuwa Siku njema ni zawadi ya msafiri.
10. Ahangaikaye sana na Jua ajua.
No comments:
Post a Comment