Amesema wafanyakazi wamekuwa waaminifu katika kulipa kodi ambayo inachangia kwenye maendeleo ya taifa kupitia mishahara yao. Alisema kwa kuwa bado vita dhidi ya wafanyakazi hewa na ufisadi inaendelea, ataangalia namna ya kuboresha mishahara yao hapo baadaye.
“Niliwaahidi wakati wa kampeni zangu kuwa nitapunguza kodi ya mapato kwenye mishahara yenu; sasa natamka kuwa nashusha kodi kutoka asilimia 11 hadi asilimia tisa. Najua punguzo hilo litakuwa limeacha pengo kwa serikali, lakini tutaangalia vyanzo vingine vya mapato vya kujazia hapo,” alisema Rais Magufuli.
Kuhusu wafanyakazi hewa, Rais amesema mpaka jana idadi ya wafanyakazi hewa imefikia 10,295. Amesema wafanyakazi hao hewa wamelipwa zaidi ya Sh 11 bilioni na kama wangeendelea kuachwa kwa mwaka mzima wangelipwa zaidi ya Sh 139 bilioni. Rais Magufuli ameapa kuwashughulika popote walipo.
Pia amewaagiza waajiri wote nchini kuwapa mikataba ya ajira wafanyakazi wao na kuhakikisha wanapeleka michango yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kukosa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano
Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani
zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la
Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili
katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya
wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment