Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, David Kafulila ameshindwa kesi ya
kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 dhidi ya mbunge wa sasa wa
jimbo hilo, Husna Mwilima (CCM) iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama
Kuu ya Kanda ya Tabora.
Kafulia
ambaye alifungua kesi hiyo mwaka jana baada ya kushindwa katika nafasi
ya ubunge na Husna Mwilima, kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Ferninand
Wambari ambaye ameamua kuifuta baada ya kutokuwepo kwa uthibitisho wa
kutosha.
Katika
kesi hiyo ambayo Kafulila aliwakilishwa na mawakili watatu, Prof.
Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera na upande wa Husna
Mwilima aliwakilishwa na wakili Kennedy Fungamtama na Mawakili wa
serikali ambao walimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
No comments:
Post a Comment