TTCL

EQUITY

Tuesday, May 10, 2016

Bilioni 59.5 zatengwa kuwawezesha Wananchi Vijijini-Serikali

SERIKALI imetenga Shilingi bilioni 59.5 katika Bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya kuwawezesha Wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa.
 
 NO.1
Taarifa hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Mahawe aliyetaka kujua ni lini fedha zingetolewa na Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia fedha hizo.
Dkt. Possi amesema kuwa, fedha hizo zitatolewa mara baada ya kuidhinishwa na Bunge hilo na baada ya kukamilisha taratibu mahususi zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo.
Ameongeza kuwa, kuhusu mpango bora wa Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi, Serikali inaendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji wa fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya Ujasiriamali.
“Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI imepewa kazi ya kuratibu utekelezaji wa mpango huo”, alisema Dkt. Possi.

No comments:

Post a Comment