Taharuki imetanda
nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye,
''kujiapishwa kama rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais
Yoweri Museveni .
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa
kizuizi cha polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na
wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika
video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana
''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa
mahakama ya juu''.
Video hiyo imesambazwa mno kwenye mitandao ya
kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda
kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za
mitandao ya kijamii.
Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya
kuwa ''endapo kutafanyika sherehe nyengine hapo kesho, basi itakuwa ni
kinyume cha sheria kwani kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi
wowote''.
Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha
upinzani cha Forum for democratic change FDC- alikamatwa na polisi kwa''
kukaidi amri halali''.
Matukio hayo yanawadia wakati ambao
viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na wageni mashuhuri wameanza
kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria kuapishwa kwa rais Museveni hapo
kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa mwezi Februari, Dr
Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi mkali nyumbani kwake baada ya
kupinga matokeo yaliyompa rais Museveni ushindi
No comments:
Post a Comment