Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe.
ALIYEKUWA mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje aliwahi
kumtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo, Wilson Kabwe
aliyesimamishwa kazi jana na Rais John Pombe Magufuli.
Wenje alitoa tuhuma hizo bungeni kwenye Bunge la 10, Mkutano wa 18,
Kikao cha 7 alipoanika namna ambavyo Wilson Kabwe alishiriki katika
usifadi wa Mradi wa Ujenzi wa Kliniki jijini humo huku akitoa maelezo
kuwa, ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Special
Audit ya mwaka wa fedha 2010/2011 ilipendekeza Kabwe achukuliwe hatua
jambo ambalo serikali halikuifanya na badala yake akahamishiwa Dar es
Salaam.
Rais John Pombe Magufuli, jana alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa
Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika
utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato
ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji
magari katikati ya jiji na kuisababishia serikali hasara ya pesa
zaidi ya bilioni 3.
Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa
daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya
Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo ripoti ya tume aliyounda kuchunguza
utekelezwaji wa mikataba hiyo.
Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe alikuwa ni
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye alihamishiwa Mwanza akitokea Mbeya
baada ya kutuhumiwa kwa ufisadi wa mabilioni kadhaa jijini humo.
No comments:
Post a Comment