Vijana
wametakiwa kugeuza changamoto kuwa fursa na kuwa na utamaduni wa
kujiajiri na kuchapakazi kwa bidii badala ya kusubiria kuajiriwa huku
wakilaumu mamlaka zinazoshughulika na vijana nchini.
Hayo
yamesemwana Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua mdahalo wa siku mbili
kujadili hatma ya ajira kwa vijana Tanzania uliyoandaliwa na Shirika la
Kimataifa la Ajira (ILO) jana jijjni Dar es Salaam.
“Changamoto
ya ukosefu wa ajira inaweza kutumika kama fursa kwa kijana
anayejitambua kwakuwa na fikra chanya itakayomuwezesha kutumia elimu
aliyoipata kujiajiri bila kuona aibu kufanya baadhi ya kazi mbali ya
kuwa amesoma hadi elimu ya juu hivyo kujiongezea kipato,”alisema Prof.
Gabriel.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Ajira (ILO) nchi
ya Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda Bi. Mary Kawar amesema
kuwa shirika hilo liko tayari kuwajengea uwezo vijana katika masuala ya
ajira ili kupunguza tatizo la ukosefuwaajira kwa vijana.
Naye
mshiriki wa mdahalo huo Bw. Masson Kimbo ameiomba serikali kupitia
mifumo ya elimu nchini itakayowawezesha vijana kujengewa uwezo wa
kujiajiri na kuwa na fikra pana katika masuala ya ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment