ALEKSANDAR VUCIC
Matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika jana nchini SERBIA
yanaonesha kuwa Waziri mkuu ALEKSANDAR VUCIC ameshinda baada Chama
chake cha Progressive Party kuongoza kwa kupata asilimia 57 ya kura
zilizopigwa.
VUCIC ambaye amekuwa waziri mkuu wa SERBIA tangu mwaka 2014 aliitisha
uchaguzi wa mapema akisema anataka kuwa na mamlaka ya kumuwezesha
kufanya mageuzi yanayohitajika ili nchi hiyo iweze kuwa mwanachama wa
Umoja wa Ulaya.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya JOHANNES HAHN alikuwa miongoni mwa
viongozi wa kwanza kumpongeza VUCIC kwa ushindi wake. SERBIA, taifa
lenye idadi ya watu Milioni Saba lilianzisha mchakato wa kujiunga na
Umoja wa Ulaya mwezi Desemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment