Mtangazaji wa Global TV Online, Adria Cleophace akimhoji mmoja wa watumiaji wa daraja
Mama ndani ya gari lake akionekana mwenye furaha kuvuka daraja la Kigamboni.
Taswira kamili.
Magari na watembea kwa miguu wakivuka.
Bodaboda nazo zikitumia daraja hilo.
Wakina mama watembea kwa miguu wakivuka.
njia za magari.
IKIWA zimebaki siku mbili tu ili Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli azindue
rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 ambalo limejengwa juu
ya Bahari ya Hindi kuunganisha kata za Kigamboni na Kivukoni, mapema hii
leo wananchi wameonekana wakitumia daraja hilo kuvuka kutoka upande
mmoja kwenda mwinguine ambapo pia magari yameonekana yakipita.
Daraja hilo ambalo limejengwa katika
mkondo wa Kurasini (Kurasini Creek), mradi huu uliobuniwa na Arab
Consulting Engineers na kujengwa na wakandarasi kampuni za China Railway
Jiangchang Engineering (T) Ltd na China Major Bridge Engineering
Company, unamilikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Sherehe za uzinduzi rasmi wa daraja hilo
utafanyika Jumanne ijayo huku mgemi rasmi atakayezindua daraja hilo
atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli.
No comments:
Post a Comment