Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akiwasili kwenye uzinduzi wa
ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report
2015) huku akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kulia) uliofanyika Machi 11,
2016 jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu) Antony Mavunde ametaka kuondolewa kwa changamoto maeneo ya
kazi ili kazi isaidie maendeleo ya binadamu badala ya kujikimu.
Naibu
Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kuzindua ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015
inayoelezea kazi kwa maendeleo ya binadamu.
Alisema
kwa sasa kuna figisu kubwa katika kazi nchini hasa kutokana na
waajiri wengi kugeuza kazi kama sehemu ya kujikimu kwa wafanyakazi wao
kwa kutowapa stahiki husika ikiwamo mikataba ya ajira.
Alisema
kazi inapokuwa ni ya kujikimu kunakuwa na migogoro mingi na kuvurugika
kwa uzalishaji na kutishia maendeleo ya taasisi husika na maendeleo ya
mtu binafsi.
Alisema
Tanzania imefurahishwa na yaliyomo katika ripoti hiyo ya Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kutokana na kuzungumzia jinsi kazi
zinavyoweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo.
Alisema
wakati Tanzania inaelekea kujipanga kwa uchumi wa kati, Ripoti
inaonyesha ni jinsi gani kazi inaweza kuboresha maisha ya Mtanzanzania
kwa kuondoa kazi na kuwapatia wananchi kazi zenye staha na zinazoweza
kuwasaidia wao binafsi na hivyo kukuza uchumi na ustawi wa jamii.
Alisema
amekuwa akizungumza katika maeneo mengi ya kazi na kukutana na
changamoto nyingi zikiwemo za kukosekana kwa mikataba, mazingira mabaya
ya kufanyakazi, ujira usiokidhi na kutaka waajiri kufuata sheria za kazi
kwa kuwapatia mikataba ya kazi na pia kuhakikisha kazi zinakuwa na
staha.
Awali
akizungumza na wageni waalikwa katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni
mwa wiki mjini Dar es Salaam, alisema kwamba uzinduzi wa kitaifa ambao
unafuatia uzinduzi wa kimataifa uliofanyika mwaka jana mjini Addis
Ababa, Ethiopia ni faraja kubwa kwa wadau wa maendeleo nchini.
Alisema
uzinduzi huo unaweka ripoti hiyo karibu zaidi na wananchi na kuahidi
serikali kuifanyia kazi kutokana na umuhimu wake hasa wa kuhakikisha
kazi inasaidia maendeleo ya watu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (kushoto) akibadilishana mawazo na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (kulia) kabla ya kuelekea kwenye uzinduzi rasmi wa ripoti ya
maendeleo ya watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015)
uliofanyika Machi 11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Anasema ripoti hiyo inaonesha namna ambavyo kazi inaweza kuchangia maendeleo na ustawi wa jamii.
Alisema
wakati Tanzania inaelekea kuwa taifa ambalo limejengeka katika msingi
wa maendeleo ya watu kama ilivyokusudiwa tangu kupatikana kwa Uhuru
wake 1961, Ripoti hiyo ni chanzo kizuri cha maarifa katika kufanikisha
mabadiliko yanayotakiwa kufanikisha maendeleo ya watu.
Alisema
kazi ni msingi wa maendeleo kwa hiyo ni vyema kuboresha mazingira ya
kazi na wafanyakazi ili kuleta maendeleo kusudiwa kwa kuwa na kazi zenye
staha.
Alipongeza
UNDP na wadau wengine kwa kufanikisha uzinduzi huo ambao alisema
umeenda sanjari na dhima ya serikali ya kutumia maarifa yote yaliyopo
kusaidia maendeleo ya watu.
Ripoti hiyo ya UNDP imetazama kwa undani kuhusu kazi, mahusiano ya kazi na maendeleo ya binadamu.
Mshehereshaji
wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human
Development Report 2015) akisherehesha uzinduzi huo uliofanyika Machi
11, 2016 jijini Dar es Salaam na kuratibiwa na ESRF.
Aidha
imeangalia masuala ya usalama wa kazi na mahitaji ya utaalamu; masuala
ya kulipwa na kutolipwa kazini, uangalizi, kujitolea ubunifu na kazi
endelevu.
Pia
ripoti hiyo inatoa majumuisha yanayostahili kufanywa bali mapendekezo
ya utengenezaji wa sera unaotanua uzalishaji kwa kutoa fursa na kulinda
wafanyakazi, ubora wa kazi, ujira stahiki, kazi yenye staha na kazi
endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kimsingi
Ripoti hiyo inapendekeza kuongeza faida za maendeleo ya binadamu,
kupitia utendaji kazi, kwa kupendekeza mikakati ya kujenga fursa za
ajira, ili kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi, na kuendeleza maeneo
yaliyolengwa, ambayo yatabadilisha hali halisi ya sasa.
Aidha
ainaangalia Sera zilizopendekezwa, kuhakikisha utendaji kazi bora,
utendaji kazi endelevu, ambayo inachangia usawa, badala ya kujenga
ukosefu wa usawa, na kazi ambayo inaheshimu haki za wafanyakazi, na
kuhakikisha usalama wao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma taarifa kwenye uzinduzi wa
Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report
2015) uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na
ESRF.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo kuna hatua njema kwenye maendeleo ya watu katika
ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwamo lakini ipo haja
ya kuangalia pengo kubwa lililopo katika fursa mbalilmbali zikiwamo za
kazi.
Imeelezwa
ndani ya ripoti hiyo kwamba toka mwaka 2000 nchi ziloizo kusini mwa
Jangwa la Sahara zimekuwa na ukuaji wa maendeleo ya binadamu( Human
Development Index -HDI) wa kazi wa kiwango cha asilimia 1.7 kati ya
mwaka 2000 na 2010 : asilimia 0.9 kwa mwaka 2010 na 2014.
HDI ni kipimo kinachotathmini maendeleo ya muda mrefu ya afya na maisha marefu, elimu na maisha yenye staha.
Kwa
Tanzania kumekuwepo na ongezeko la HDI la asilimia 1.18% kati ya
mwaka 1985 na 2014, ikiongezeka kutoka 0.371 hadi 0.521, ikiwa ni
ongezeko la asilimia 40.5 juu ya ongezeko la nchi zilizo kusini mwa
Jangwa la Sahara la 0.518.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (hayupo pichani) kuhutubia wageni
waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya
mwaka 2015 (Human Development Report 2015) uliofanyika jijini Dar es
Salaam Machi 11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Mratibu
wa Umoja wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza katika
uzinduzi huo alisema kwamba ongezeko hilo si haba.
Hata
hivyo aliwaambia wadau waliokuwepo kushuhudia uzinduzi huo kwamba Taifa
bado linakabiliwa na changamoto nyingi zikkiwemo umaskini uliokithiri,
kutanuka kwa pengo la usawa na kushindwa kuhimili matukio ya mabadiliko
ya tabianchi na uchumi.
Aidha
alisema kwamba :”Ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015,
inaonyesha kuwa, kuimarisha maendeleo ya binadamu, kupitia utendaji
kazi, inahitaji sera na mikakati katika maeneo makuu matatu: kujenga
fursa za ajira, kuhakikisha ustawi wa wafanyakazi na kuendeleza maeneo
yaliyolengwa. Hii inaongeza kasi ya kutengeneza ajira nchini Tanzania.”
Tanzania
ikiwa na zaidi ya watu milioni 12 wakiishi katika umaskini na wengi wao
uliokithiri changamoto kubwa kwa Tanzania, ni kutafsiri uwezo huu
katika miundombinu inayoonekana, kwa kujenga mazingira mazuri, na
kuongeza ujuzi wa watu wake kama ilivoainishwa katika Ripoti ya
Maendeleo ya Binadamu mwaka elfu mbili na kumi na tano.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akisoma hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya
Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwa
niaba ya Waziri Jenista Mhagama, uliofanyika jijini Dar es Salaam Machi
11, 2016 na kuratibiwa na ESRF.
Alisema
changamoto zote hizo ni za kweli na zenye uhusiano na maendeleo ya
binadamu na ni vyema ilivyowekwa katika Muono wa maendeleo ya Tanzania
kufikia 2025 na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Katika
hotuba yake ya shukurani Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo,
alisema kwamba taasisi yake ipo tayari kusaidia Tanzania na nchi
nyingine kuwezesha kutambua uhusiano kati ya kazi na maendeleo ya
binadamu katika utekelezaji wa Maendeleo endelevu (SDGs).
Mgeni
rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) na meza kuu
wakijiandaa kuzindua ripoti hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi,
Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi
Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report
2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 2016.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akionyesha ripoti hiyo kwa
wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti
hiyo.
Muonekano wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015). Kwa picha zaidi bofya link hii
No comments:
Post a Comment