Baadhi
ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo
vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa
Makumbusho Sekondari.
Taasisi
mpya ya Kijamii ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo
ya kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza
imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na
kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.
Tukio
hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia
Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na
Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa
shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto
wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.
Madam
Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu
mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi
hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad
Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul
Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye
mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni
ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.
“Madam
Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji
maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi
hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu
usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa
vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu
ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja”
alieleza Madam Sophy.
Madam
Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi
zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu
wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma hivyo jukumu lililopo ni
kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza
miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata
maeneo muhimu.
Aidha,
Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki
tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo
alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua
pamoja na kuwasaidia wenzake.
Madam
Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu, ni miongoni mwa wanafunzi waliopata
kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002
ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani
na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika
kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa
ni moyo.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye
aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akitoa
nasaha zake kwa niaba ya Mh. Masauni. wakati wa uzinduzi rasmi wa
taasisi hiyo ya Madam Sophy Charity Events. Upande wa kulia ni Madam
Sophy.
Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Wakovu wanaosimamia shule hiyo ya Msingi wakifuatilia tukio hilo..
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika mkutano huo.
Wageni waalikwa.
Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani)
Mtoto
Emmanuel Anthony 'Rais' akifurahia jambo katika tukio hilo. Emmanuel
ameeleza kuwa, licha ya kuwa mlemavu, ndoto yake ni kuja kuwa Rais.
Meja
wa Wilson Chacha wa Jeshi la Wokovu ambaye pia aliwahi kumfundisha
Sophy miaka ya nyuma akitoa salamu zake katika tukio hilo
Mtoto akisoma risala maalum kwa mgeni rasmi
Mgeni
rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akikata keki
kwa pamoja na Madam Sophy kuashiria uzinduzi rasmi wa tukio hilo.
Mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa akimlisha keki Madam Sophy.
Madam Sophy akimlisha keki mgeni rasmi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa
Madam Sophy akimlisha keki mama yake mzazi wakati wa tukio hilo..
Mama Mzazi wa Sophy akimkumbatia mwanae
Mwanadada,
Hoyce Temu aliyejitoa kusaidia watanzania kupitia kipindi maalum cha
'MIMI NA TANZANIA' akilishwa keki na Madam Sophy katika tukio hilo
Hoyce Temu akimpongeza Madam Sophy kwa kuanzisha taasisi hiyo pamoja na kuandaa shughuli hiyo
Madam Sophy akitoa nasaha zake juu ya hatua aliyofikia hadi kuanzisha taasisi hiyo.
Baadhi ya watoto waliofika katika tukio hilo wakifanya maombi maalum kuwaombea wenzao wenye mahitaji maalum.
baadhi ya watoto hao wenye ulemavu wa viungo
Madam Sophy akitoa nasaha zake
Madam
Sophy akikabidhi baadhi ya zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Makumbusho
ambayo anafundisha pamoja na watoto wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu.
No comments:
Post a Comment