SERIKALI ya Awamu ya tano chini
ya Rais Dk. John Magufuli imeombwa kuviangalia kwa ukaribu vituo vya kulelea
watoto yatima na wasiojiweza kwa kuvipatia ruzuku ili viweze kujiendesha vyenyewe tofauti na
hivi sasa vinategemea misaada kutoka kwa wasamaria wema.
Rai hiyo ilitolewa na Bi. Jenipher Massawe mmoja wa walezi wa watoto wenye ulemavu wa akili na wasiojiweza wa Kituo cha Building Caring Community (BCC) alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wetu, katika mmoja ya vituo 11vilivyopo chini ya kanisa la KKKT usharika wa Moshi Mjini.
Bi. Jenipher Massawe akizungu na watoto |
Aliongeza kusema, kituo kimekua kikitoa mikopo ya gharama nafuu, yenye riba ya 6% kwa wazazi wa watoto wote wenye ulemavu, na kufanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kufichua watoto wenye ulemavu waliofungiwa ndani na kutoa mafunzo/ elimu kwa jamii kuhusu madhara ya kuwaficha watoto wao.
Aidha alimalizia kwa kutoa wito kwa serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa inavikumbuka vituo vyote vya kulea watoto yatima, na wasiojiweza katika kuwapatia ruzuku na miasaada mbalimbali kwakua vimekuwa vikifanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii, hususa kaya masikini na zenye watoto walemavu, ambapo wengi wao huenda wangekuwa ombaomba na watoto wa mitaani.
No comments:
Post a Comment