TTCL

EQUITY

Wednesday, March 2, 2016

Mkutano wa EAC umeanza leo Jijini Arusha

Viongozi Wakuu wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wameendelea kuwasili Jijini Arusha ambapo mapema jana Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein pamoja Rais wa Uganda Yuweri Museven, waliwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa na Rais Yoweri Museveni,Uhuru Kenyatta na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein
Tayari mwenyeji wao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alikwishawasili Jijini Arusha tokea Jumamosi iliyopita ya Februari 28 tayari kwa mkutano wa 17 wa viongozi wakuu wa EAC unaotarajiwa kufanyika Ngurdoto nje kidogo ya Jiji la Arusha hii leo.
Rais wa Zanzibar Dkt Shein aliwasili katika kiwanja cha ndege cha KIA mapema jana na baadaye Rais Museven wa Uganda naye akawasili kiwanjani hapo na kupokelewa kwa heshima zote na viongozi mbalimbali pamoja na kushuhudia burudani za ngoma kutoka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harson Mwakyembe akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao amesema tayari ajenda mbalimbali zitakazozungumzwa na viongozi hao zimeshaandaliwa na kwamba kikao cha baraza la mawaziri kutoka nchi wanachama kimekwishakamiliki.
Baada ya mkutano wakuu hao wa Mataifa ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kushiriki zoezi la uwekwaji wa jiwe la msingi la ukarabati wa barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi kesho, ukarabati unaofanywa na mkandarasi HANIL-JIANGSU JOINT

No comments:

Post a Comment