Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimelalamikia
kukamatwa kwa baadhi ya wabunge na madiwani wao wa jiji la Dar es
salaam na kusema kuwa kitendo hicho ni hujuma zinazofanywa na watawala.
Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe
Akizungumza
jana katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho mwenyekiti wa taifa wa
chama hicho Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa anahisi wakati viongozi hao
wakishikiliwa uchaguzi utaishwa wakati makada wao wakiwa kizuizini.
Mhe Mbowe amesema kuwa hatua ya kukamatwa viongozi hao ni hujuma za kisiasa zinazoendelea ambapo pia kumekua na mikakati ya kuzigawa manispaa wanazoziongoza ili Chama cha Mapinduzi kiweze kuchukua nafasi katika halmashauri mpya.
Wabunge wanaoshikiliwa na polisi mpaka sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Mhe. Halima Mdee. Mbunge wa Ukonga Mhe. Mwita Waitara pamoja na madiwani wawili lakini pia Mbunge wa jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea anaendelea kutafutwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

No comments:
Post a Comment