Alfajiri
ya leo Jumatano, daladala linalotokea Gongo la Mboto kuelekea
Mawasiliano limegongana na lori lilivyokuwa limebeba Ng’ombe na lori la
mizigo, ajali hiyo imetokea eneo la Darajani kabla ya kufika Tabata
Matumbi.
Mmoja
wa shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema kuwa daladala ilikuwa
imejaza abiria na baada ya kufika eneo hilo yaligongana na kusababisha
vifo vya baadhi ya abiria waliokuwa katika daladala hiyo.
Taarifa kamili zitafuata baadae.
No comments:
Post a Comment