Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mbarawa, ameelezea kutoridhishwa kwake na utendaji kazi wa
Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa) juu ya uendeshaji wa vivuko na
ukusanyaji mapato.
Sambamba na hilo, ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
kubadilika kiutendaji ili kujiendesha kibiashara badala ya kutegemea
serikali.
Akizungumza jana na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini hapa, Profesa
Mbarawa, alisema serikali itachukua uamuzi mgumu ikiwamo kuwachukulia
hatua wale wanaoshindwa kuwajibika.
Alisema wizara ilitangaza kutumia Sh. bilioni 60 kufanya
matengenezo na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Musoma ili
kuwaondolea adha wananchi wa mkoa na watalii wanaofika kutembelea
hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Alisema hatua hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa
Hayati Mwalimu Julius Nyerere, hivyo serikali imetenga dola
milioni 30 (zaidi ya Sh. bilioni 60 kwa ajili ya kazi hiyo.
Aliongeza ulegevu katika kazi umesababisha adha kubwa kwa
wananchi ambao sasa wanalazimika kusafiri hadi mkoani Mwanza
kutafuta huduma hiyo huku uwanja huo ukikosa mapato.
Kuhusu Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Profesa Mbarawa alisema
inapaswa kubadilika kiutendaji badala ya kutegemea serikali kufanya
biashara ili kuongeza pato la taifa.
Hivi karibuni, Profesa Mbarawa alianza kazi ya kusafisha taasisi
Zilizo chini ya wizara yake kwa kuwang’oa vigogo waandamizi wa Mamlaka
ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (THA) na kuwahamishia makao makuu ya
wizara. Pia alimsimamisha kazi meneja wa Fedha wa Kampuni ya Ndege
Tanzania (ATCL) kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha.
No comments:
Post a Comment