TTCL

EQUITY

Friday, February 19, 2016

Matokeo ya awali Uganda Museveni anaongoza

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Uganda inaendelea na kazi ya kuyatangaza matokeo ya uchaguzi wa urais na ubunge uliofanyika hapo jana.

Matokeo hayo ni ya awali katika vituo 1247 kati ya vituo 28010 ambayo ni sawa na asilimia 36.58% ya kura ambazo zilizopigwa.
Matokeo yanaonyesha kwamba Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni anaongoza kwa kura 2191283 sawa na asilimia 62.03% akifuatiwa kwa mbali na kiongozi wa upinzani Dkt. Kizza Besgye ambaye amepata kura 1182025 sawa na asilimia 33.4% huku wagombea wengine wakigawana idadi iliyobaki.
Aidha waangalizi wa umoja wa ulaya wameelezwa kusikitishwa na jinsi zoezihilo lilivyoendeshwa huku kiongozi wa upinzani Dkt. Kizza Besigye akikamatwa mara kadhaa na jeshi la polisi nchini humo.

No comments:

Post a Comment